Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Angalia Picha :TUNDU LISSU ATIKISA SHINYANGA AKIZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI CHADEMA KANDA YA SERENGETI...MAELFU WAJITOKEZA, APEWA UCHIFU

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu akihutubia maelfu ya wanachama wa CHADEMA na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga katika Uwanja wa Joshoni Mjini Shinyanga katika uzinduzi wa  Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Maelfu ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga na mikoa jirani wamejitokeza katika uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu kwenye Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara.

Tundu Lissu aliyekuwa ameambatana na Mgombea Mwenza, Salum Mwalimu, Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Esther Matiko, Mgombea Ubunge Jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya na Mgombea Ubunge jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba,baadhi ya wagombea ubunge na udiwani Kanda ya Serengeti amefanya uzinduzi rasmi wa Kampeni za Uchaguzi Kanda ya Serengeti leo Jumatano Septemba 2,2020 katika Uwanja wa Joshoni Mjini Shinyanga.

Mara baada ya kuwasili uwanjani, Lissu alipokelewa na Wazee wa Kabila la Wasukuma kisha kumfanyia maombi na dua maalumu, kumvalishwa vazi maalumu, kukabidhiwa mkuki wa ushindi na usinga na kiti cha kifalme/kichifu na wazee wa kabila la Kisukuma huku akipewa Uchifu na kupewa jina la Chifu Ng’waya.

Baada ya kumaliza kufanya uzinduzi wa Kampeni za CHADEMA Kanda ya Serengeti majira ya saa 12 jioni, Tundu Lissu alielekea katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti huku akisindikizwa na wafuasi wa CHADEMA ambao walifurika nje ya ofisi hizo na kutawanyika baada ya Tundu Lissu na msafara wake kuondoka katika ofisi hizo majira ya moja na dakika 26 usiku.

Akinadi Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA inayosisitiza Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu, Tundu Lissu alisema serikali ya CHADEMA itazingatia masuala ya haki kwa kila mwananchi na kuhakikisha kila mmoja anafaidi matunda ya nchi na kwamba anataka kila mmoja awe na pesa mfukoni. 

Tundu alisema endapo CHADEMA itashinda katika uchaguzi mkuu 2020 atahakikisha analeta mapinduzi katika sekta ya kilimo na ufugaji ili kila mwananchi anufaike na kilimo na ufugaji na kwamba ataondoa kodi zinazoumiza wananchi.

Kwa upande wake,Mgombea Mwenza wa Urais CHADEMA, Salum Mwalimu aliwaomba Watanzania kutochukulia uchaguzi mkuu kama ushabiki wa Simba na Yanga bali ni mustakabali wa maisha yao hivyo wasifanye makosa wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na kumchagua Tundu Lissu kuwa Rais wa Tanzania pamoja na wabunge na madiwani wa CHADEMA.

Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe aliwataka Watanzania kuchagua viongozi watakaokwenda kusimamia haki huku akiwasihi Wagombea kupitia CHADEMA wakiwemo Wabunge na Madiwani kufanya kampeni za kistaarabu na wananchi kutafakari na kufanya uamuzi sahihi badala ya kufanya masihara kwani uchaguzi ndiyo mustakabali wa maisha yao.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, John Mnyika alisema taifa linakwenda kumpata Rais atakayekwenda kusimamia haki ya nchi na maendeleo ya rasilimali katika maeneo mbalimbali, hivyo akawaomba wananchi na wafuasi wa chama hicho kuwapa kura za ushindi madiwani na wabunge wote wa Kanda ya Serengeti ili kumsaidia Tundu Lissu kupata wasaidizi makini.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu na Mgombea Mwenza Salum Mwalimu (mbele) wakiwapungia mkono wakazi wa Shinyanga baada ya kuwasili katika Uwanja wa Joshoni Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuzindua rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu leo Jumatano Septemba 2,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu akisalimiana na viongozi wa CHADEMA Kanda ya Serengeti na wazee wa kabila la Kisukuma baada ya kuwasili katika Uwanja wa Joshoni Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuzindua rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu leo Jumatano Septemba 2,2020.

Wazee wa Kabila la Kisukuma wakimvalisha na kumpatia vitendea kazi vya Kichifu Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu 'Aliyepewa jina la Chifu Ng'waya' baada ya kuwasili katika Uwanja wa Joshoni Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuzindua rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu leo Jumatano Septemba 2,2020.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu 'Chifu Ng'waya'  akionesha vitendea kazi vya Kichifu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Joshoni Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuzindua rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu leo Jumatano Septemba 2,2020
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu 'Chifu Ng'waya'  akifurahia baada ya kupewa Uchifu wa Kabila la Kisukuma.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu akiwahutubia wanachama wa CHADEMA na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga katika Uwanja wa Joshoni Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 

Sehemu ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu akiwahutubia wanachama wa CHADEMA na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga katika Uwanja wa Joshoni Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu akihutubia maelfu ya wanachama wa CHADEMA na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga katika Uwanja wa Joshoni Mjini Shinyangawakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu  
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe akizungumza katika Uwanja wa Joshoni Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga ,kupitia CHADEMA, Salome Makamba (kushoto)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu akimuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga ,kupitia CHADEMA, Salome Makamba (kushoto).
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe akizungumza katika Uwanja wa Joshoni Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
Mgombea Mwenza Urais CHADEMA Salum Mwalimu akizungumza katika Uwanja wa Joshoni Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 

Mke wa Tundu Lissu akimuombea kura mme wake achaguliwa kuwa Rais wa Tanzania wakati wa uzinduzi Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
 Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyikaakizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
Mgombea Ubunge jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba,Mgombea Ubunge Jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Esther Matiko wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
Viongozi wa CHADEMA wakiwa kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
Wananchi na wafuasi wa CHADEMA wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
Wanachama wa CHADEMA na wananchi wakiwa kwenye  uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 

Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 

Moja ya mabango yanayoonesha namna ya kuchangia Kampeni za Tundu Lissu.
Wananchi wakiendelea kuchangia Kampeni za Tundu Lissu
Zoezi la kuchangia Kampeni za Tundu Lissu likiendelea
Wanachama wa CHADEMA na wananchi wakiwa kwenye  uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
Wanachama wa CHADEMA na wananchi wakiwa kwenye  uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
Wanachama wa CHADEMA na wananchi wakiwa kwenye  uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
Wanachama wa CHADEMA na wananchi wakiwa kwenye  uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
Wanachama wa CHADEMA na wananchi wakiwa kwenye  uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu akiondoka katika uwanja wa Joshoni Shinyanga Mjini baada ya kuzindua Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 Kanda ya Serengeti.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu akiwaaga kwa kuwapungia mkono wananchi waliojitokeza katika uwanja wa Joshoni Shinyanga Mjini kushuhudia uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 CHADEMA Kanda ya Serengeti.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu akiwasili katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya kuzindua Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 CHADEMA Kanda ya Serengeti.
Wafuasi wa CHADEMA na wananchi wakiwa nje ya ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu kuwasili katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya kuzindua Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 CHADEMA Kanda ya Serengeti.

Wafuasi wa CHADEMA, wananchi na Askari polisi wakiwa nje ya ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu kuwasili katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya kuzindua Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 CHADEMA Kanda ya Serengeti.
Wafuasi wa CHADEMA na wananchi wakiwa nje ya ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu kuwasili katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya kuzindua Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 CHADEMA Kanda ya Serengeti.
Wafuasi wa CHADEMA na wananchi wakiwa nje ya ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu kuwasili katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya kuzindua Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 CHADEMA Kanda ya Serengeti.
Wafuasi wa CHADEMA na wananchi wakiwa nje ya ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu kuwasili katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya kuzindua Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 CHADEMA Kanda ya Serengeti.
Wafuasi wa CHADEMA na wananchi wakiwa nje ya ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu kuwasili katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya kuzindua Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 CHADEMA Kanda ya Serengeti.
Wafuasi wa CHADEMA na wananchi wakiwa nje ya ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu kuwasili katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya kuzindua Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 CHADEMA Kanda ya Serengeti.

Wafuasi wa CHADEMA na wananchi wakiwa nje ya ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu kuwasili katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya kuzindua Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 CHADEMA Kanda ya Serengeti.
Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tundu Lissu ukiondoka katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti baada ya kuzindua Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 CHADEMA Kanda ya Serengeti.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com