Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (katikati) akiwaelezea viongozi wa dini mkoani Geita mradi wa soko la dhahabu pamoja na vyumba vya biashara vilivyofadhiliwa na GGML kwa ushirikiano na Halmashauri ya Mji Geita.
Mwenyekiti wa umoja wa Dini Mkoani Geita Askofu Stephano Saguda(katikati) akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa kuwatembeza katika ziara hiyo na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Kampuni ya GGML pamoja na Serikali katika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo Mkoani Geita.
NA
MWANDISHI WETU
VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani
Geita wamefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoani humo
na kueleza kufurahishwa na usimamizi dhabiti miradi hiyo kwa maendeleo ya
Tanzania.
Viongozi hao wamefanya ziara hiyo ambayo imedhaminiwa
na Kampuniya Geita Gold Mining Limited (GGML) pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Geita kwa lengo la kuona na kupata ufafanuzi wa miradi inayotekelezwa mkoani
humo.
Akizungumzia ziara hiyo iliyofanywa leo, Mkuu wa
Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel alisema ofisi yake inatambua mchango mkubwa
wa viongozi wa dini katika kutunza amani na umoja ndani ya jamii.
“Huwezi kupata maendeleo katika jamii yoyote bila kuwa
amani. Amani inayotupatia maendeleo katika nchi yetu na mkoa wetu wa Geita
inalindwa na viongozi wa dini ambao siku zote wamekuwa
na ushawishi kwa waumini wao kuhubiri amani,” alisema
Aidha,
Meneja Miradi inayofadhiliwa na Geita Gold Mining Limited (GGML) kupitia fedha za
Wajibu wa Kampuni kwa Jamii (CSR) Bw Moses Rusasa alisema katika ziara hiyo kuwa
lengo la Kampuni ya GGML ni kuhakikisha jamii inayozunguka mgodi inafaidika.
“Tunatekeleza
miradi mingi ndani ya mkoa wa Geita kwasababu mojawapo ya tunu inayoongoza Kampuniya
GGML ni kufaidisha jamii inayotuzunguka. Katika ziara hii na viongozi wa dini, tumetembelea
Soko la Dhahabu, Soko la Katundu pamoja na kituo cha uwekezaji (EPZA) miradi ambayo
imefadhiliwa na Kampuni ya GGML kwa maendeleo ya watu wa Geita,” alisema Bw Rusasa.
Akitoa
neno la shukrani wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Dini Mkoani
Geita, Askofu Stephano Saguda alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa kuwatembeza
katika ziara hiyo na kumpongeza kwa kazi nzuri ya kusimamia maendeleo katika Mkoa
wa Geita.
“Tunampongeza
sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Magufuli kwa kuupatia
Mkoa wa Geita kiongozi makini anayesimamia maendeleo. Nawapongeza pia Kampuni ya
GGML kwa kushirikia na vyema na Serikali hususani Halmashauri za Geita na kutekeleza
miradi mikubwa yenye gharama kubwa katika Mkoa wa Geita,” alisema Askofu Saguda.
Kwa
miaka 10 iliyopita, GGML imewekeza Jumla ya Dola Milioni 25 kutekeleza miradi mbalimbali
ya maendeleo Mkoani Geita na Tanzania kwa ujumla. Mkakati ni kutenga pia Dola Milioni
53 kwa ajili ya miaka 14 ijayo.