KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI ATOA RAI KWA TAASISI ZOTE NCHINI KUWA NA BAJETI ZA KUWAWEZESHA WAHITIMU FANI YA UHANDISI

 Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Katibu mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ametoa rai kwa taasisi zote  nchini kuhakikisha zinakuwa na Mpango kabambe wa kutenga bajeti ili kuwawezesha wahitimu wa vyuo vikuu  wa fani ya uhandisi kujishikiza katika taasisi hizo mara tu wanapohitimu kabla ya kupata ajira kuliko kuzurura mtaani.


Mhandisi Sanga amebainisha hayo Septemba 4,2020  jijini Dodoma katika akifunga mkutano Mkuu wa 17 wa Mwaka wa Wahandisi uliokwenda na kaulimbiu isemayo "Katika mapinduzi ya 4 ya Viwanda  vipi uelekeo katika kukabiliana na changamoto za dunia"

"Katika kutoa motisha na kuwapa moyo vijana kuipenda fani ya uhandisi ni lazima  kuangalia mbinu pindi wanapohitimu wasiwe wa kuzurura njia sahihi ni kuwaandalia mazingira hivyo ni vyema taasisi kuaandaa bajeti ya kuwawezesha kujishikiza katika taasisi hizo kabla ya kuajiriwa kuliko kuwaacha wanazurura mtaani kwani fani ya uhandisi ni nyeti mno kwa maendeleo ya taifa"amesema.

Aidha,ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wahandisi  waliokula kiapo cha uaminifu kuhakikisha wanazingatia maadili ya taaluma yao .

Pia Mhandisi Sanga amewapongeza Wahandisi kote nchini kwa kufanikisha Tanzania kuivusha katika uchumi wa kati na kubainisha kuwa uwezo waliojengewa Wahandisi katika mkutano huo utakuwa chachu kwa maendeleo ya Taifa.

Kuhusu ufuatiliaji,Mhandisi Sanga ameitaka bodi ya Usajili ya Wahandisi kuhakikisha inafuatilia kwa makini na muafaka maazimio kwa ajili ya kufanya mrejesho baadae .
Mwenyekiti wa bodj ya Usajili ya Wahandisi Mhandisi Prof .Ninatubu Lema amesema karibu washiriki 3500 wameshiriki mkutano huo wa Mwaka wakiwamo washiriki 500 waliokuwa wakifuatilia kwa njia ya mtandao kutoka maeneo tofauti ya dunia.

Hali kadhalika Prof.Lema amebainisha baadhi ya mapendekezo yaliyotokana na mkutano huo kuwa ni pamoja na kuwa na chombo kitakachokuwa kinashauri upande wa Effort(Kanda),uhitaji wa kubadili mitaala ya Elimu kuanzia chini hadi juu ili taifa linufaike na mapinduzi ya Viwanda .

Prof. Lema ametaja mapendekezo mengine ni pamoja na kuifanya Dodoma kuwa jiji la mfano kwa kupendeza na miundombinu iliyobora (Smart City),kuhamasisha Sera ili ziende kwenye Usajili na ziweze kutekelezwa 

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wahandisi  kote nchini,Mhandisi Mohammed Jaye kutoka  Zanzibar ameshukuru kwa Serikali  kwa kuendelea kuimarisha mkutano kwa kila Mwaka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post