Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Singida imemhukumu adhabu ya kutumikia kifungo cha maisha jela mkazi wa Mtaa wa Minga katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Husein Azizi (34) baada ya kukiri kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka minne.
Baada ya kusomewa shtaka lake, mshtakiwa huyo amekiri na kudai hakuwa akifanya kitendo hicho kwa mtoto huyo peke yake bali kulikuwa na mtoto mwingine ambaye aliyefanyanae kitendo hicho bila kugundulika.
Kwa mujibu wa mwanasheria huyo, mshtakiwa Azizi amedai, watoto hao walikuwa wakimfuata hadi machungani kutokana na kuwa walimpenda sana na hakuwa amefanya tendo hilo mara moja bali alikuwa akifanya mara kwa mara.
Mwanasheria wa Serikali, Elizabeth Barabara amedai kuwa, mshtakiwa alitenda kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka minne Agosti 6, 2020 mtaa wa Minga.
Akitoa hukumu ya kesi hiyo ya jinai namba 135/2020, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Robert Oguda amesema ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama ya mshitakiwa huyo, atahukumiwa kwenda kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Social Plugin