Katika hali isiyotarajiwa, Ann Magwi na Jonathan Munini, kutoka Tana River Kenya, wamelazimika kukatisha zoezi la kufunga ndoa, baada ya James Sidai kujitokeza kanisani na kusema yeye ndio Baba yao Mzazi.
Baba huyo aliingia kanisani akiwa na Dada yake na kusema ndoa hiyo isifungwe kwa kuwa Maharusi ni Ndugu wa damu.
“Mama zenu nyie, mmoja aliniacha akaondoka na mtoto akiwa na mwaka mmoja, mwingine aliona uchumi wangu umeyumba akaondoka akiwa na mimba ya miezi minne na akaolewa na mwalimu, nikaamua kumuoa mwingine na tuna watoto watatu, nimeona tangazo la harusi yenu WhatsApp zile picha nikasema hawa ni wanangu nikachunguza kwa watu mlioishi nao wakasema ni kweli,” amesema James.
Bwana harusi ambaye ni mfanyabiashara katika mji wa Madogo aliondoka kanisani kwa hasira akimuacha mama yake akiwa analia huku bibi harusi akiondoka na mama yake ambaye inadaiwa alikuwa amepoteza fahamu.
Social Plugin