MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati alipotembelea mradi wa Maji Michokeni wilayani Pangani wakati wa ziara yake kulia ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella na katikati ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ziara hiyo
MSIMAMIZI wa Mradi wa Maji unatoa Maji kutoka Pongwe hadi Muheza Adela Mboya akielezea jambo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela wakati wa ziara yake
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alipotembelea mradi wa maji Pongwe unaopeleka maji wilayani Muheza
TATIZO sugu la uhaba wa maji katika wilaya nne za mkoani Tanga linatarajiwa kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kufuatia Serikali kuwa na mpango wa kutekeleza mradi mkubwa utakaogharimu sh 100. bilioni.
Wilaya zitakazonufaika na mradi huo utakaotoa maji katika mto Pangani ni Pangani,Muheza,Korogwe na Handeni.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela amesema hayo wakati wa ziara yake yakukagua miradi ya maji inayosimaniwa na Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Jiji la Tanga Tanga UWASA katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Amesema Kuwa ujio wa miradi hiyo katika mkoa huo utaweza kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji kwa zaidi ya asilimia 90% hali ambayo itasaidia kuimarisha uchumi wa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo amesema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa maeneo ya Vijiji ni asilimia 65% wakati katika maeneo ya mjini ni asilimia 18%pekee.
Amesema kuwa ukamilikaji wa miradi ya maji utaweza kuongeza kiwango cha huduma hiyo hadi kufikia asilimia 52% na hivyo kusaidia kupunguza kwa kiasi fulani Changamoto ya ukosefu wa maji katika wilaya hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira Jiji la Tanga Tanga UWASA Geofrey Hilly amesema kuwa kukamilika kwa mradi wa maji kutoka Pongwe kwenda Muheza kutasaidia huduma ya maji hadi katika Vijiji vya jirani katika maeneo ambayo mabomba ya maji yatapita.
Social Plugin