Zana hizo zilizokuwa zinatumika katika uvuvi haram zimekamatwa wakati wa operesheni za kawaida za kudhibiti uvuvi haram Wilayani Busega na kubaini uvunjifu mkubwa wa sheria na taratibu za uvuvi unaofanywa na baadhi ya wavuvi, alisema Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Busega Bw. Mwita Mokeha.
Licha ya kuteketeza zana haram za uvuvi pia baadhi ya wavuvi wanaofanya uvuvi haram wameweza kupigwa faini na kupewa onyo kali kufanya shughuli za uvuvi haram ili iwe fundisho kwa wavuvi wengine wasiofata sheria na taratibu za uvuvi. Zana hizo haram zimeteketezwa baada ya kupata idhini ya mahakama, aliongeza Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Busega, Bw. Mokeha.
Uvuvi haram katika Ziwa Viktoria umekuwa ukifanywa na baadhi ya wavuvi na kusababisha upunguaji wa samaki katika ziwa hilo, na kupelekea upotevu mkubwa wa mapato ya halmashauri yatokanayo na shughuli za uvuvi. Kwa upande mwingine imebainika kwamba baadhi ya wavuvi wamekuwa na uelewa mdogo kuhusu shughuli za uvuvi hivyo hupelekea kufanya uvuvi haram.
MWISHO