Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HESLB YAFUNGA DIRISHA LA MAOMBI YA MIKOPO 2020/2021..... MAOMBI 92,947 YAPOKELEWA NA KUSAJILIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru (katikati) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari Agosti 31 mwaka huu kuhusu kuongezwa kwa muda katika dirisha la maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2020/21. Kushoto ni Meneja Masoko wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Joseph Kimaro na kulia ni Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Mwanaisha Said.
 (PICHA NA BODI YA MIKOPO- HESLB)

******* 

TAARIFA KWA UMMA
 KUFUNGWA KWA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA 2020/2021


1.0       UTANGULIZI

Tunafahamisha wadau wote kuwa kuwa leo Alhamisi (Septemba 10, 2020) saa 6:00 usiku dirisha la upokeaji wa maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2020/2021 kwa njia ya mtandao, litafungwa rasmi. Baada ya muda huo, usajili mpya kwa ajili ya maombi mapya hautaruhusiwa.

2.0       MUDA WA UOMBAJI KWA NJIA YA MTANDAO

Tarehe 21 Julai, mwaka huu, HESLB ilifungua dirisha la maombi ya mkopo kwa njia ya mtandao na kisha kufuatia maombi ya wazazi, walezi na wanafunzi, muda wa maombi ya mkopo uliongezwa kwa siku 10 hadi leo Septemba 10, 2020 saa sita usiku. Mpaka mchana wa leo, jumla ya maombi 92,947 yamesajiliwa na kupokelewa yakiwemo maombi 7,500 yaliyopo katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji.

HESLB inatoa wito kwa waombaji mikopo 7,500 wenye maombi yasiyokuwa na viambatisho muhimu, kukamilisha maombi hayo haraka iwezekanvyo ili yaweze kujumishwa kwenye tathmini na uchambuzi.

3.0       DIRISHA LA UHAKIKI WA MAOMBI KWA WAOMBAJI MIKOPO

Uhakiki wa taarifa za maombi ya mikopo, utaanza tarehe 1 Oktoba na kisha HESLB itaorodhesha maombi yaliyobainika kuwa na kasoro mbalimbali kupitia katika mfumo.

4.0       WITO KWA WADAU WA HESLB

Kwa kuzingatia kuwa mchakato wa maombi ya mikopo unahusisha wadau mbalimbali, HESLB inawasisitiza wadau inaoshirikiana nao ikiwemo Shirika la Posta Tanzania (TPC) kuendelea kuwahudumia waombaji mikopo wote kwa kupokea na kutuma maombi yao kwa kuzingatia mwongozo wa uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021.



6.0     BAJETI KWA MWAKA WA MASOMO
         
Serikali kupitia HESLB, imetenga kiasi cha TZS Bilioni 464 kwa ajili ya wanafunzi 145,000, ambapo kati yao wanafunzi wanufaika 54,000 watakuwa wa mwaka wa kwanza na 91,000 ni wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo.

7.0       HITIMISHO

HESLB inawashauri wazazi, walezi na wanafunzi kuendelea kufuatilia vyanzo rasmi ikiwemo tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) kuhusu taarifa muhimu na orodha ya watakaopangiwa mikopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021 na kwa mujibu wa kalenda ya mwaka wa kitaaluma (academic almanac) ya mwaka huu.

Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru,
Mkurugenzi Mtendaji,
10 Septemba, 2020,
DAR ES SALAAM.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com