Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

IRAN YAIONYA MAREKANI DHIDI YA KOSA LOLOTE LA KIMKAKATI BAADA YA KITISHO CHA TRUMP

Iran imeionya Marekani  dhidi ya kufanya makosa ya kimkakati, baada ya rais Donald Trump kuitishia Tehran, kuhusiana na ripoti kwamba inapanga kulipiza kisasi mauaji ya jenerali wake wa juu Qasem Soleimani.


Msemaji wa serikali ya Iran Ali Rabiei amesema katika mkutano na waandishi habari uliotangazwa kupitia televisheni, kwamba wanatumai Marekani haitafaya makosa hayo na iwapo watayafanya, watashuhudia majibu thabiti ya Iran.

Trump aliapa jana kwamba shambulizi lolote la Iran litakabiliwa na majibu ambayo ukubwa wake utakuwa mara 1,000 zaidi, baada ya ripoti kwamba Iran inapanga kulipa kisasi cha mauaji ya jenerali Qasem Soleimani.

Ripoti ya vyombo vya habari nchini Marekani, ikinukuu maafisa ambao hawakutajwa majina, ilisema mpango wa Iran kumuuwa balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini ulikuwa unasukwa kuelekea uchaguzi wa rais wa Marekani mwezi Novemba.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com