Katiba ya Kenya inataka sheria hiyo kuwepo ili kudhibiti jinsia bungeni kutotawala katika nyadhifa za uteuzi, na kwa miaka 10 sasa wabunge ambao wengi ni wakiume, wameshindwa kupitisha sheria hiyo.
Hatua hiyo ya Jaji Mkuu inaungwa mkono na chama cha Mawakili nchini humo na idadi kubwa ya wabunge wanawake ambao ni asilimia 22 katika baraza la bunge la kitaifa na asilia 22 katika Bunge la Senate.
Jaji Maraga amesema wabunge na maseneta wamekwenda kinyume cha Katiba ya mwaka 2010 iliyowataka kutunga sheria hiyo.
Spika wa bunge la kitaifa, Justin Muturi ameiambia Televisheni ya nchi hiyo ya Citizen kuwa, hatima ya Bunge hilo sasa ipo mikononi mwa rais Kenyatta.