Jaji Mstaafu Mark Bomani ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanzania amefariki dunia usiku wa kuamkia leo September 11, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole ameandika kupitia Twitter “Chama Cha Mapinduzi tumepokea kwa huzuni taarifa ya kifo cha Jaji (Mst) Mark Bomani, MwanaCCM & Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanzania, Uongozi unatoa pole kwa familia, wafiwa & wote walioguswa na msiba huu. Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe”
Social Plugin