KITANDULA AAHIDI NEEMA MKINGA,KUPELEKA UMEME NGAZI YA VITONGOJI


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Duga Maforoni wilayani Mkinga wakati wa uzinduzi wa kampeni zake
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula kulia akipokea kitabu cha ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu wakati alipozindua kampeni za Ubunge Jimbo hilo eneo la Duga Maforoni wilayani Mkinga
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula kulia akipokea kitabu cha ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu wakati alipozindua kampeni za Ubunge Jimbo hilo eneo la Duga Maforoni wilayani Mkinga
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Mkinga kulia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Dastan Kitandula

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula akiwa ameshika ilani ya CCM mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu wakati wa uzinduzi wa kampeni wa Jimbo hilo
MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Tanga Dkt Aisha Kigoda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hizo
MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Husna Sekiboko akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Mwantumu Zodo akisisiitiza jambo wakati wa uzinduzi huo

MJUMBE wa Halmashauri Kuu Taifa (MNEC) kupitia kundi la UWT Taifa Catherine Kitandula akizungumza wakati wa uzinduzi huo

SEHEMU ya wana CCM na wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo
SEHEMU ya wana CCM na wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo

SEHEMU ya wana CCM na wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Meja Kunta akitumbuiza wakati wa kampeni hizo



MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mkinga mkoani Tanga (CCM) Dastan Kitandula amezindua rasmi kampeni zake huku akiwaomba wananchi kumchagua tena kuwatumikia kwa kipindi cha miaka mitano ili aweze kumalizia kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.


Kero kubwa ambazo zimekuwa zikilikabili Jimbo hilo ni suala la Maji na barabara ambapo alihaidi kuzipatia ufumbuzi wa kina wakati atakapopewa ridhaa ya kuwatumikia wananchi hao

Uzinduzi wa Kampeni hizo ulifanyia kwenye Kijiji cha Duga Maforoni wilayani humo ambapo ilizinduliwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu.


Alisema wakati akipata ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2000 Jimbo hilo lilikuwa nyuma kimaendeleo lakini hadi sasa asilimia 90 ya vijiji vimeunganishiwa umeme wa Rea na miradi ya maji, barabara na elimu imetekelezwa kwa asilimia kubwa.


Alisema hivi sasa baadhi ya vijiji ambavyo vilikuwa vikikabiliwa na uhaba wa maji wananchi wanapata maji safi na salama na kutolea mfano wa kijiji cha Mapatano.


Mgombea huyo alisema Kijiji cha Doda wakazi wake wame unganishiwa maji kupitia mradi wa mabwawa uliogharimu sh 1.4.bilioni wakati kata ya Duga Sigaya wananchi wanapata maji kutokana na mradi wa sh 1.2 bilioni.

Kitandula ambaye anatetea kiti hicho alisema iwapo atachaguliwa tena kushika ubunge wa jimbo hilo atahakikisha anatia msukumo Serikalini

ili mradi mkubwa wa kutoa maji Mabayani Jijini Tanga na kuyafikisha hadi mpaka wa Tanzania na Kenya wa Horohoro unatekelezwa.


Akizungumzia suala la umeme, Kitandula alisema wilaya ya Mkinga ina jumla ya vijiji 85 ambapo 65 vimesha unganishiwa nishati hiyo huku vijiji 20 vilivyobaki vikiwa vipo katika hatua za mwisho za mchakato wa kupatiwa umeme kupitia REA.


“Mkinichagua kushika nafasi hii nitahakikisha umeme sasa unapelekwa ngazi ya vitongoji vilivyopo katika vijiji vyote 85 na mtandao wa barabara utaongezeka zaidi”alisema Kitandula.


Kitandula amepewa dhamana ya kupeperusha bendera ya CCM kuwaniaubunge wa jimbo la Mkinga ambapo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 28 atapambana na Nuru Bafadhil wa CUF na Rehema Ali Mohamed wa ACT-Wazalendo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post