LIGI KUU MSIMU WA 2020/21 KUANZA SEPTEMBA 6 MWAKA HUU

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Pazia la Ligi Kuu Msimu wa 2020/21 Linafunguliwa tena mapema wikiendi hii kwa viwanja vitano nyasi zake kuwaka moto.

Msimu mpya wa Ligi unatarajia kuanza Septemba 06 mwaka huu.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limezitaka klabu zote za Ligi Kuu msimu huu zenye wachezaji wa kigeni pamoja na watumishi wengine wasio raia wa Tanzania kupeleka vibali vyao vya kazi ili kupata uthibitisho.

  Katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu utakaopigwa katika Uwanja wa Majaliwa Mkoani Lindi utawakutanisha Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Namungo dhidi ya Coastal Union, huku Biashara United ikiwakaribisha Gwambina kwenye Uwanja wa 

Timu ya Ihefu iliyopanda Ligi Kuu msimu huu baada ya kuwaondoa Mbao Fc kwenye mchezo wa Play off itawakaribisha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Simba katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, wakati huo huo Dodoma Jiji wakiwa nyumbani dhidi ya Mwadui 

Katika mchezo wa mwisho utakaopigwa ndani ya dimba la Mkapa itawakutanisha Yanga dhidi ya Tanzania Prisons.

Kila timu imejinasibu kuweza kufanya vizuri katika msimu huu wa Ligi Kuu 2020/21 je nani kunyakua ubingwa wa msimu huu.??


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post