Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBWANA SAMATTA AJIUNGA NA KLABU YA FENERBAHCE YA UTURUKI


Mshambuliaji wa timu ya soka nchini Tanzania Mbwana Samatta amejiunga na klabu ya Uturuki Fenerbahce kwa mkataba wa miaka minne kutoka Aston Villa.

Klabu hiyo imeandika katika mtandao wake kwamba imemuongeza nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania katika kikosi chake kwa mkataba wa miaka minne.

Mchezaji huyo aliyeshinda taji la mfungaji bora mara kadhaa nchini Ubelgiji kabla ya kujiunga na Aston Villa nchini Uingereza atahudumu katika klabu hiyo kwa mkopo wa mwaka mmoja kabla ya kuandikisha kandarasi ya kudumu ya miaka minne.

Ripoti kutoka Istanbul zinasema kwamba mshambuiaji huyo atavalia jezi nambari 12 mgongoni katika klabu yake mpya.

Fenerbahce inayoshiriki katika ligi kuu ya Uturuki siku ya Ijumaa ilimzindua Samatta rasmi ikichapisha kanda ya video katika akaunti yake ya Twitter .


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com