Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA SAU AAHIDI AJIRA, KUNUNUA NDEGE KILA MKOA NA KUIMARISHA KILIMO

Chama cha Sauti ya Umma (SAU) kimezindua Ilani na kampeni zake kwa ajili uchaguzi unaotarajia kufanyika Oktoba 28, mwaka huu, huku kikiahidi kuwa endapo kitashika dola huo utakuwa mwisho ma matumizi ya jembe la mkono nchini na kila mkoa utakuwa na ndege yake kwa ajili ya kubeba abiria.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ilani na kampeni za chama hicho jana, jijini Dar es Salaa, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Muttamwega Mgaywa alisema ilani ya chama hicho imelenga kuikomboa nchi kupitia kilimo na viwanda.

Alisema chini ya uongozi wa Serikali ya SAU, hakuna mkulima atakayelima Kwa kutumia jembe la mkono, badala yake trekta ndizo zitakazotumika ili kumpunguzia mzigo kwa mkulima.

Pia aliahidi kuwa chini ya Serikali ya chama hicho, wanawake watakuwa wakijifungua bure. 


Aidha, ameongeza kuwa iwapo atachaguliwa ataendeleza kazi nzuri iliyofanywa na marais waliopita hususani awamu ya tano

Kuhusu suala la aridhi na Maywa amesema kila Mtanzania atamiliki ardhi bila gharama yoyote.

Kwa upande wake mgombea mwenza wa chama hicho, Satia Musa Bebwa amewahakikishia vijana wanaomaliza elimu ya juu kupata mitaji itakayowawezesha kuingiza kipato.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com