Maandalizi ya kumpokea mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida Dkt John Pombe Magufuli yamekamilika.
Akizungumza jana na waandishi wa habari juu ya maandalizi hayo Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu alisema maandalizi yamekamilika ambapo leo wanatarajia kumpokea Mgombea huyo mkoani hapo.
Alisema pamoja na maandalizi yote mgombea huyo atahutubia wanachama na wananchi pamoja na kunadi ilani ya chama hicho ya mwaka 2020-2025 ambayo alisema imejaa shehena ya vitu vizuri,pia atapata fursa ya kuwatambulisha na kuwanadi wagombea nafasi ya ubunge katika majimbo nane ya mkoa huo.
Social Plugin