Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Mwinyi, amesema ataimarisha sekta ya utalii ili vijana wapate ajira na kuongeza pato la taifa.
Alisema ataboresha maisha ya wajasiriamali, wafanyabiashara wadogo wakiwamo waendesha bodaboda.
Dk. Mwinyi alitoa ahadi hiyo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Aliwataka wananchi kumchagua yeye pamoja na wagombea wote wa CCM, ili kuendeleza kuwaletea naendeleo.
Social Plugin