NAIBU Waziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema kuwa wananchi wa Tanzania hawana sababu ya kutokipigia Kura Chama Cha mapinduzi CCM kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano.
Naibu waziri wa Kilimo Mgumba amebainisha hayo wakati akizungumza katika kikao Cha Halmshauri Kuu Maalum ya Wilaya ya Morogoro Vijijini,iliyokutana kwa ajili ya kuwaleta wanachama wa CCM pamoja ili kuhakikisha chama hicho kinaibuka na ushindi wa kishindo kuanzia udiwani ,Ubunge na Urais.
Mgumba ambaye aligombea kuteuliwa kuwa mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na kupata Kura 242, ambapo Hamis Taletale (Babu Tale ) alibuka mshindi na kuwa mgombea wa Ubunge wa Jimbo hilo na kwa sasa ni mbunge mteule kutokana na kupita bila kupingwa katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki
Omary Mgumba amesema sasa ni wakati wa kuondosha makundi ya kisiasa kwa kuhakikisha chama Cha Mapinduzi CCM kinapata Ushindi wa kutosha.
Mgumba pia amesema Innocent Kalogelesi Mbunge Mteule wa Morogoro Kusini na Hamis Taletale wa Morogoro Kusini Mashariki wana nafasi kubwa ya kuhakisha hakuna makundi mara baada ya kumaliza kwa michakato ya kumpata atakayepeperusha bendera katika majimbo ya Morogoro Kusini,na Kusini Mashariki.
Katika hatua nyingine amesema kuwa watahakikisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt. John Magufuli anapata kura za kutosha kutoka majimbo hayo.
Amesema wanaimaani kubwa kuwa majimbo hayo yataongoza kwa kumpigia kura Magufuli kutokana na kile ambacho amekifanya ndani ya Miaka mitano.
Sanjari na hilo ameongeza kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 imegusa sekta zote muhimu zenye kuja kumkomboaa mwananchi.
Nao baadhi ya waliokuwa watia nia katika majimbo hayo wameahidi kuungana na walioteuliwa na kuwa kitu kimoja ili kuhakiksha Chama Cha Mapinduzi CCM kinapata kura za kutosha katika majimbo ya Morogoro kusini,na Kusini Mashariki hasa katika Urais kutokana na tayari kuna wabunge wateule.
Social Plugin