Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAFUNZI 10 WAFARIKI DUNIA BAADA YA BWENI KUUNGUA MOTO KAGERA


Picha ya bweni la wavulana lililoungua Moto na kusababisha wanafunzi 10 kufa papohapo kayika shule ya msingi Byamungu Islamic English Medium iliyopo Itera wilayani Kyerwa Kagera.
***
Na Emmanuel Ndosi - Kagera
Shule ya Msingi Byamungu Islamic iliyoko Kata ya Itera wilayani Kyerwa mkoani Kagera, imeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Septemba 14, 2020.


Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya hiyo Rashid Mwaimu amesema kuwa watoto 10 wamethibitika kupoteza maisha.

Bweni hilo la wavulana lilikuwa na wanafunzi 74.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amewasili eneo la tukio, ambapo wakati akizungumza kwa njia ya simu amesema mbali na vifo hivyo pia kuna majeruhi saba, na kwamba ameunda tume itakayochunguza tukio hilo.

Gaguti ameagiza shule hiyo ifungwe kwa muda na wanafunzi wote warudi majumbani mpaka watakapoamriwa kurudi tena.

Pia amesena serikali itagharamia mazishi ya wote waliopoteza maisha pamoja na kuwatibu wote waliojeruhiwa  kwenye mkasa huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com