Mratibu wa Huduma za mama na mtoto Manispaa ya Musoma, Deborah Mkama akimuelekeza mama jinsi ya kumnyonyesha mtoto wakati wa mafunzo ya namna ya unyonyeshaji ya Mother Meet Up Event yaliyoandaliwa na Shirika la FHI360 chini ya ufadhili wa Shirika la misaada la Marekani la USAID mjini Musoma jana.
Baadhi ya akinamama wakifuatilia mafunzo juu ya namna bora ya kunyonyesha sambamba na suala zima la malezi ya mtoto, mafunzo hayo yaliyofanyika mjini Musoma jana ambayo yakiitwa Mother Meet Up event huku yakiandaliwa na Shirika la FHI360 chini ya ufadhili wa Shirika la misaada la Marekani la USAID.
Baadhi ya akinamama wakifuatilia mafunzo juu ya namna bora ya kunyonyesha sambamba na suala zima la malezi ya mtoto, mafunzo hayo yaliyofanyika mjini Musoma jana ambayo yakiitwa Mother Meet Up event huku yakiandaliwa na Shirika la FHI360 chini ya ufadhili wa Shirika la misaada la Marekani la USAID.
Halmashauri ya Manispaa ya Musoma na Rorya mkoani Mara zanufaika na mradi wa USAID Tulonge Afya unaolenga kutoa elimu katika jamii ili kubadili tabia hasi ili kuweza kuisaidia jamiii kuwa na Afya njema..
Akizungumza mjini hapa jana kwenye shughuli ya wakina mama wenye watoto chini ya miezi sita ijulikanayo kama “Mother Meetup” iliyoandaliwa na na mradi wa USAID TULONGE AFYA kupitia jukwaa la NAWEZA kwa lengo la kuwakumbusha wakinamama hao juu ya malezi bora ya watoto .
Mratibu wa asasi ya OWSL, Dk. Theophil Kayombo dhumuni la kuwakutanisha kina mama hao ni kuwapa nafasi ya kuweza kupeana uzoefu na kujadiliana mambo mbalimbali yahusuyo malezi ya watoto kuanzia wanapozaliwa mpaka kufikia umri wa miaka mitano.
Aidha Dkt, Kayombo aliainisha mambo hayo kuwa ni Umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama pekee yake kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo bila kumpatia mtoto vyakula vya ziada , baada ya kujifungua umuhimu wa kutumia njia za kisasa za Afya ya UZAZI ili kuzuia kupata mimba nyingine ndani ya miaka miwili.
Ili kuruhusu mtoto kukua na kuwa na afya bora , kuhakikisha mama na Mtoto mchanga analala ndani ya chandarua kilichotiwa dawa ili kujikinga na ugonjwa wa Malaria, pamoja na umuhimu wa kumpeleka mtoto mchanga katika kituo cha kutolea huduma za afya mara tu unapogundua dalili za ugonjwa.
Ameongeza kuwa kupitia mradi wa Tulonge Afya wanawafikia jamiii kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na uundwaji wa vikundi,elimu kwa njia mbalimbali lengo likiwa ni kuwafikia walengwa katika makundi yao ili waweze kuelimika na kufuata kanuni bora za afya kama inavyoelekezwa na wataalam.
Mratibu wa uhamasishaji huduma za jamii kutoka ofisi ya mganga mkuu wa manispaa ya Musoma, Dk. Magreth Shaku aliishukuru asasi hiyo kwa kuamua kutekeleza mradi huo ndani ya manispaa ya Musoma kwa maelezo kuwa mradi huo umekuja muda muafaka hivyo utasaidia katika kuongeza uelewa wa jamii juu ya masula mbalimbali ya afya ikiwemo suala la kunyonyesha watoto hasa katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo mtoto anapozaliwa.
Dk. Shaku alisema kuwa suala la unyonyeshji wa watoto bado linakabaliwa na changamoto mbalimbali zinazopelekea akinamama kushindwa alkunyonyesha kama inavyoshauriwa kitaalam hali ambayo kwa namna moja ama nyingine imekuwa ikileta changamoto katika suala zima la makuzi ya mtoto.
Alizitaja baadhi ya changamoto kuwa ni pamoja na baadhi ya akinamama kukataa kunyonyesha watoto wao wakidai kuwa maziwa yao yataanguka pamoja na ushiriki hafifu wa akinababa kwenye suala zima la malezi ya mtoto.
Aliwataka akinamama kuhakikisha kuwa wananyonyesha watoto ipasavyo kwa maelezo kuwa mbali na unyonyeshaji kuwa na manufaa katika makuzi ya watoto lakini pia ni njia kuu mojawapo ya kumkinga mama dhidi ya ugonjwa wa saratani ya matiti.
Naye mratibu wa mradi huo, Cyprian Lungu, alisema Mradi wa USAID Tulonge Afya ni mradi miaka mitano unatekelezwa na serikali kwa kushirikiana na shirika la FHI360 na wadau wengine chini ya ufadhili wa shirika la kimarekani lijulikanalo kama USAID. Mradi huu unatekelezwa hapa nchini katika Wilaya 29 kwenye mikoa 12. Kwa upande wa mkoa wa Mara mradi unatekelezwa katika wilaya mbili ambazo Musoma Manispaa na Rorya
Aliongeza kuwa mradi huo unalenga kuleta mabadiliko ya tabia kwa kupambana na tabia hasi katika jamii zinazouia wanajamii kupata huduma bora za afya.
Alisema kuwa akinamama watapata elimu juu ya namna wanavyotakiwa kujiandaa kiafya kabla na baada ya kujifungua pia namna bora ya kuwalea watoto wao katika umri wa chini ya miaka mitano jambo ambalo litasaidia kuwa na jamii iliyo bora.