Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu, akionesha ngao na mikuki aliyokabidhiwa na wazee wa kimila ikiwa ni ishara ya ushindi.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu, akihutubia wakati akiomba ridhaa ya kuongoza jimbo hilo kwa miaka mitano katika mkutano wa hadhara wa kufungua kampeni za uchaguzi uliofanyika Stendi Mpya ya Mabasi ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida jana.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu, akiwasili viwanja vya mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Viongozi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa (kushoto) akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Siasa, Edward Mpogolo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi Elibariki Kingu, akimtuza Msanii wa kugani mashairi maarufu kwa jina la Kiherehere.
Wagombea udiwani wa jimbo hilo kupitia CCM wakiserebuka.
Wasanii wakitoa burudani.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi Elibariki Kingu (kushoto), Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida, Mashariki Miraji Mtaturu (katikati) na Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe wakiserebuka baada ya kupagawishwa na Msanii maarufu wa nyimbo za Sengeli Mzee wa Bwax.
Msanii maarufu wa nyimbo za Sengeli Mzee wa Bwax, akitoa burudabi kwenye mkutano huo.
Umati wa watu katika mkutano huo.
Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, akizungumza katika mkutano huo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akitema cheche wakati akimuombea kura, Rais Magufuli, Mtaturu na madiwani wa jimbo hilo.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa, akizungumza kwenye mkutano huo.
Wagombea udiwani wakitambulishwa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba, akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu Mwenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu (kulia) akiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wanachama kati ya 28 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliohamia CCM wakitambulishwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Miraji Mtaturu amesema siasa sio kama ushabiki wa Simba na Yanga au Timu ya Manchester na Arsenal bali ni maisha yetu wa Tanzania.
Mtaturu aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara wa kufungua kampeni za uchaguzi za Jimbo la Singida Mashariki uliofanyika Stendi Mpya ya Mabasi ya Wilaya ya Ikungi mkoani hapa na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi na wana CCM.
" Siasa ni maisha yetu..tunapo zungumzia siasa tunazungumzia maji, barabara, umeme, elimu na miundo mbinu. Nawaomba ndugu zangu uchaguzi wa mwaka huu tusiufanye kama ushabiki wa mpira." alisema Mtaturu.
Alisema uchaguzi ni wa muhimu sana kwa sababu kwa miaka mitano kulikuwa na mambo ambayo waliyatamani wayapate lakini leo na wao ni mashahidi kwamba kuna mambo yalikuwa hayaendi na baadhi ya wapinzani wao walikuwa wakiulalamia mwenendo wa Serikali yetu na sasa wamekosa maneno na kuanza kuyabadilisha na kusema miundombinu inayojengwa sasa eti ilijengwa tangu nchi yetu inapata uhuru na kuwa eti sio muhimu kuwa na barabara za lami, kuwa na ndege wakati ndio waliokuwa wakisema tangu tupate uhuru miaka 60 nchi haijawahi kuwa na hata na shirika la ndege.
Alisema kuwa ni wapinzani hao hao ndio waliokuwa wakizungumzia katika miaka hiyo 60 vijiji havina umeme, huku maji safi na salama ikiwa bado ni ajenda, lakini Rais John Magufuli amekuja na kuwa tiba na ameweza kusimamia rasilimali za nchi na na kufanikiwa huku akirudish nidhamu ya Serikali.
"Mwaka 2015 tuliwaambia mchagueni huyu Magufuli na kuwa ataweza kutuvusha leo katika miaka mitano hii tuna jivunia uongozi wake bora." alisema Mtaturu.
Alisema Rais Magufuli amewagusa hata wao wana Singida Mashariki kwani leo wanapofanya tathmini ya miaka mitano wanajiona wamesonga mbele walikuwa na changamoto ya maji wakina mama walikuwa wakienda mbali kutafuta maji lakini sasa ndani ya jimbo hilo tayari wamechimba visima vya maji 15 ambavyo vipo katika vijiji mbalimbali na wamebakiza vijiji vitatu tu kati ya 12 na Rais amewapa Sh.bilioni 2 kwa ajili ya kukamilisha mradi huo wa maji akimaanisha akipewa tena miaka mingine mitano anakwenda kumaliza changamoto walizokuwa nazo wananchi wa jimbo hilo kwa miaka mitano iliyopita.
" Mimi nilipoingia nilikwenda kuchochea kazi ambayo ilianza kufanywa katika miaka mitano iliyopita niwaombe sana wanapokuja watu kuwaomba ridhaa ya kuongoza tuwapime kwanza namna wanavyoeleza kwani baadhi yao wanakuja kitapeli kwa nia ya kutaka kutugonganisha na kuwatia hasira wananchi kwamba Rais na Serikali haifanyi vizuri hivyo na waambia muachane nao" alisema Mtaturu huku akishangiliwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano huo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi Elibariki Kingu, Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa waliwaomba wananchi hao kuwapigia kura za kutosha kwa mgombea nafasi ya Urais Dkt . John Magufuli, Miraji Mtaturu pamoja na madiwani wa chama hicho.
"Tunawaomba wana Ikungi tumpe kura nyingi Mtaturu kwani kwa kipindi cha miezi tisa aliyokaa katika nafasi hiyo ameweza kutuletea miradi mingi ya maendeleo kama maji, umeme wa REA, Chuo cha Veta, Hospitali ya Wilaya ambayo ujenzi wake utakamilika miezi miwili ijayo miradi ambayo haikuweza kufanyika kwa miaka yote wakati jimbo hilo likiwa chini ya wapinzani" alisema Kingu.
Kwa upande wake Mattembe alisema kama kwa miezi hiyo tisa Mtaturu ameweza kutekekeza miradi hiyo je akipewa ridhaa ya kuongoza tena kwa kipindi cha miaka mitano si atafanya mambo makubwa zaidi ya hapo.
Katika mkutano huo wanachama 28 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) wa Jimbo la Singida Mashariki John Sililo, walirudisha kadi za chama hicho na kujiunga na CCM ambapo walipokelewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba.