NDUGAI AFUNGUA SHINA LA WAKEREKETWA CCM LA WAFANYA BIASHARA IPEMBE SINGIDA

Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa Ndugu Job Ndugai Akihutubia wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wa shina na 3 la Ipembe mkoani Singida.
 Eneo la Shina la wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi CCM  Mbacho Guest ambalo lipo kata ya Ipembe Manispaa ya Singida.
 Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa Ndugu Job Ndugai akiwakabidhi kadi za CCM wanachama wapya waliohamia Chama Cha Mapinduzi CCM kutoka vyama vingine vya upinzani.
Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa Ndugu Job Ndugai akiwakabidhi kadi za CCM wanachama wapya waliohamia Chama Cha Mapinduzi CCM kutoka vyama vingine vya upinzani.

Na Ismail Luhamba, Singida.


MJUMBE wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Job Ndugai amesema Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania linatarajia kuboresha sheria kwa wafanyabiashara nchini ili wafanye biashara zao kwa tija.


Mjumbe huyo ambaye pia ni Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyasema hayo jana wakati akizindua shina la wakereketwa wa CCM ambao ni wafanyabiashara kata ya Ipembe Wilaya ya Singida mjini. 

Ndugai alitumia nafasi hiyo kuwaomba wanachama wote na wasio wanachama siku ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura na kukipigia chama cha CCM kwani kina mambo makubwa ya kimaendeleo kwa wananchi wake.

Awali akisoma taarifa fupi ya shina hilo kabla ya kuzinduliwa, atibu msaidizi wa shina hilo Florian Malya alisema wafanyabiashara hao wanaiomba serikali kuwawekea mazingira mazuri ya kufanikisha biashara zao ili waweze kujipatia kipato na kuweza kulipa kodi mbalimbali kwa mujibu wa sheria.

"Sisi wafanyabiashara tunakiunga mkono chama cha Mapinduzi na tutahakikisha kinashinda kwa kishindo kwa ngazi zote kuanzia diwani,mbunge na Rais",alisema Malya.

Shina hilo ambalo lipo eneo la Mbacho Guest kata ya Ipembe lina wanachama 50 likiwa linaongozwa na mwenyekiti wake Philipo Masawe, katibu ni Mark Kimboka na katibu msaidizi akiwa ni Florian Malya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post