MBUNGE Mteule Viti Maalum kundi la Asasi za kiraia Tanzania
bara kwa tiketi ya CCM Neema Lugangira, amesema kuwa atakuwa
kiunganishi kati ya Asasi za kiraia(NGO'S), bunge, serikali, wafadhili
na chama ili kubadilishana mawazo katika kuleta maendeleo endelevu.
Neema ameyasema hayo wakati alipotembelea Mtandao wa
Vikundi vya wakulima wadogo Tanzania (MVIWATA) mkoani Morogoro ili kujua
changamoto zinazo wakabili na namna ya kuzitatua.
Ameeleza kuwa kwa kuongea na wadau hao anapata fursa ya
kupata mambo ya kujadili yaliyomo kwenye ilani ya CCM yanayohusiana na
Asasi hizo na kuweza kubadilishana mawazo yatakayosaidia kwenye
utekelezaji.
Akizungumzia maeneo yaliyoguswa na ilani ya CCM amesema
lengo kubwa ni kuongeza tija katika kilimo ili kusaidia viwanda,
kuimarisha miundo mbinu na uzalishaji, kumsaidia mkulima kuzalisha na
kupata masoko, usimamizi wa mazao ya kimkakati, lishe na kuzijengea
uwezo Asasi za ndani.
Naye Mkurugenzi wa MVIWATA Stephen Ruvuga akitoa shukrani
zake kwa chama na serikali amesema kwa kitendo hicho cha kiongozi
kuwatembelea na kujua changamoto zao wanatarajia kuwepo kwa maelewano
mazuri kati ya serikali na Asasi hizo, hali itakayochochea maendeleo kwa
haraka.
Social Plugin