MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa Kata ya Duga Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni |
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa Kata ya Duga Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni |
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimnadi mgombea udiwani wa Kata ya Duga (CCM) |
MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Tanga Dkt Aisha Kigoda akimuombea kura kwa wananchi wa Kata ya Duga mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu |
Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mwatumu Mahiza akimuombea Kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM)Ummy Mwalimu |
KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo kapange akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa mkutano huo |
MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Mhandisi Mwanaisha Ulenge |
Umati Mkubwa wa wananchi wakimsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu(CCM)
Msanii wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo
Msanii wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atapigania maboresho ya awamu ya pili ya Bandari ya Tanga ili kuongeza fursa za ajira na kuongeaza vipato vya wakazi wa Jiji hilo.
Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa Kata ya Duga Jijini Tanga katika mkutano wake wa kampeni alisema huo ni mkakati wake wa kutaka kuona meli kubwa zinatia nanga kwenye bandari hiyo.
“Ndugu zangu wana Duga naombeni kura zenu niweze kulibadilisha Jiji la Tanga kwa kuhakikisha tunasukuma maboresho ya awamu ya pili ya Bandari ya Tanga kuweza kuongeza fursa za ajira kwa vijana”Alisema
Alisema pia licha ya uwepo wa fursa za ajira kwa vijana lakini pia vipato vya wakazi wa mji wa Tanga vitaongezeka kutokana na mzunguko mkubwa wa biashara .
“Katika hili tunamshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kutuwezesha milioni 372 kwa ajili ya maboresha ya awamu ya kwanza ya Bandari hiyo lengo langu ni kutaka bandari ya Tanga meli kubwa zote ziweze kutia nanga kwenye bandari”Alisema
Alisema meli hizo kubwa zikitia nanga kwenye Bandari hiyo itawawesha vijana waweze kupata ajira wanaume na wanawake na mji utachangamka na hivyo kuchochea kipato cha mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
“Nitumeni Bungeni ninaaminika ninaweza kupiga hodi kwa kiongozi yoyote, waziri yoyote ili bandari ya Tanga iweze kuboreshwa na kuweza kufungua fursa za ajira kwa vijana wanawake na wanaume “Alisema
Hata hivyo alisema kwamba amedhamiria kupigania mizigo yote inayokwenda mikoa ya kanda ya kaskazini ishushwe kwenye bandari ya Tanga badala ya Dare s Salama ili mji huo uweze kuchangamsha .
“Hili nitalipigania usiku na mchana ili kuweza kurejesha heshima ya Jiji la Tanga nataka kuona mji huu unapata mafanikio makubwa na kuwa kama Singapori.