Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inapenda kuwataarifu waombaji wa nafasi za ajira ya Madaktari zilizotangazwa na Serikali mwezi Agosti, 2020 kuwa zoezi la uchambuzi wa maombi yaliyopokelewa limekamilika.
Aidha, waombaji wa nafasi za ajira ya Madaktari waliokidhi vigezo wamepangiwa kazi katika Vituo vya Afya na Hospitali mbalimbali za Wilaya/Halmashauri nchini.
Madaktari wote waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa kuanzia tarehe 23 Septemba, 2020 hadi 30 Septemba, 2020. Aidha, waombaji watakaoshindwa kuripoti kwenye vituo vya kazi kwa tarehe hizo bila ya taarifa, nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa haraka iwezekanavyo.
2. Kuwasilisha kwa waajiri wao (Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa) vyeti halisi (Originals Certificates) kwa ajili ya kuhakikiwa na waajiri kabla ya kupewa barua za ajira. Vyeti hivyo ni kama ifuatavyo:
(i) Cheti cha kuzaliwa;
(ii) Cheti cha Kidato cha Nne na Sita/Diploma;
(iii) Cheti cha Kuhitimu Shahada ya Udaktari;
(iv) Cheti cha Usajili wa Baraza la Madaktari Tanzania (MCT); na
(v) Uthibitisho wa Kumaliza Mazoezi kwa Vitendo (Internship).
3. Kwa Madaktari waliosoma nje ya nchi wanatakiwa kuwasilisha vyeti vya ithibati (Accreditation Certificates) kutoka NACTE/TCU.
Orodha ya Madaktari waliopangiwa vituo vya kazi katika Halmashauri mbalimbali nchini inapatikana kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz.
Limetolewa na:-
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais - TAMISEMI,
DODOMA.
22 Septemba, 2020
Kuona majina ya waliochaguliwa bofya <<HAPA>>
Social Plugin