MSAJILI
wa Hazina, Athumani Mbuttuka akizungumza wakati wa hafla ya kufunga
mafunzo ya semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta
nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni
Kondo,akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya semina
elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta nchini yaliyofanyika
kwa siku tano, jijini Dodoma.
Postamasta
Mkuu Hassan mwang'ombe,akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya
semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta nchini
yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano) Kitolina Kippa,akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo
ya semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta nchini
yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
Kaimu
Meneja Mkazi POSTA Zanzibar Bw.Khamis Swedi,akitoa neno la shukrani kwa
Mgeni rasmi Msajili wa Hazina Athumani Mbuttuka (hayupo pichani) wakati
wa hafla ya kufunga mafunzo ya semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa
Shirika la Posta nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
Sehemu
ya washiriki wa mafunzo ya semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa
Shirika la Posta nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
MSAJILI
wa Hazina, Athumani Mbuttuka akiwa katika picha ya pamoja na washiriki
mara baada ya kufunga mafunzo ya semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa
wa Shirika la Posta nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
.................................................................................
Na.Alex Sonna,Dodoma
MSAJILI
wa Hazina, Athumani Mbuttuka amelitaka Shirika la Posta Tanzania kuweka
mikakati ya kutengeneza faida zaidi ili kuongeza gawio kwa serikali.
Aidha,
ameitaka Bodi ya Shirika hilo kuweka vigezo maalum vya kupima utendaji
kazi wa Mameneja wa Mikoa kwenye makusanyo ili watakaoshindwa kukidhi
waondolewe.
Mbuttuka,
ameyasema hayo leo alipokuwa akifunga mafunzo kwa viongozi wa shirika
hilo nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
Amesema
kila tawi la shirika hilo lihakikishe linapata faida na washindane kwa
kadri faida inavyotengenezwa ili kuongeza gawio kwa serikali.
“Hili
gawio la Sh.Milioni 350 kwa ukubwa wa shirika hili, haiwezekani,
tunatarajia kwa muda mfupi ujao tuanze kuzungumzia Bilioni na tunajua
inawezekana,”amesema.
Hata hivyo, amesema kuna kamati yake ya ufundi inatengeneza mikataba ambayo itakuwa na malengo ya kupima shirika hilo.
“Tunataka
tukikupima tukupime kwa kitu sahihi, katika muda mfupi ujao mtapata na
kusaini mikataba mipya ili kuhakikisha kwamba shirika la posta linafanya
kwa ufanisi kulingana na vigezo vya kupima ufanisi,”amesema.
Mbuttuka amepongeza shirika hilo kwa kutengeneza faida chanya tofauti na ilivyokuwa awali.
“Kwa miaka mitatu mfululizo mmejitahidi kutoa gawio miaka miwili mmetoa
Sh.Milioni 350 kila mwaka, ule mwaka mwingine mmetoa Sh.Milioni 250,
mnajua haitoshi, hivyo muweke mikakati ya kuongeza,”amesema.
Aidha,
Msajili huyo amesema vimewekwa vigezo vya gharama za uendeshaji ambapo
zinatakiwa zisizidi asilimia 50 lakini bado Shirika linajiendesha kwa
gharama ya asilimia 75.
Naye,
Posta Masta Mkuu Shirika hilo, Hassan Mwang’ombe, amesema mafunzo hayo
yameweka mwelekeo mmoja wa utendaji kazi ambao kuna viwango vya ufanisi
vimewekwa ambapo kila Meneja wa Mkoa anatakiwa awe amezalisha asilimia
75 ya bajeti Shirika.
Amesema
dhamira ya shirika hilo ni kwa kinara cha utoaji huduma na kuna
mikakati mbalimbali ya kufikia azma hiyo ambayo itaongeza utoaji wa
gawio kwa serikali.