Shirika la Tanzania Nuru ya Amani (TANUA) linalofanya shughuli zake za kuhamasisha amani na kuratibu kampeni za kitaifa zenye kulenga kuinua uchumi wa Tanzania na kipato cha wananchi kupitia miradi mbalimbali, leo Tarehe 26 Septemba wamefungua Kampeni maalumu inayolenga kuhamasisha utalii wa ndani ya nchi.
Katika uzinduzi huo, Mgeni rasmi alikuwa Bi Upendo Massawe Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa Ibanda-Kyerwa ambaye ameambatana na viongozi wa TANAPA na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii nchini.
Uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha utalii wa ndani umeambatana na kutangazwa rasmi tarehe ya matembezi ya utalii wa hifadhi ya taifa ya Ibanda itakayofanyika tarehe 01 January 2021.
Akifungua kampeni hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Shirika la TANUA lenye Makao makuu yake Arusha, Ndg Justiniani Kazunguru Amesema lengo la kitengo hiki cha utalii ni kuhakikisha watanzania wanahamasika kulipa kodi kwa vitendo kupitia kitengo cha utalii nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Shirika la TANUA, Ndg Justiniani Kazunguru |
Mwenyekiti wa Shirika la TANUA nchini Ndg Enock Bujuli amewaomba viongozi wa dini waliowakilishwa na Sheikh wa wilaya Karagwe Ndg Nasibu Abdul, Askofu wa Kanisa la TAG Mch Elias Manoti na Mchungaji James Kakuru wa kanisa la The fountain of life church Tanzania (chemichemi) Kuhamasisha waumini na watanzania kuthamini vya kwao na kuendeleza utamaduni halisi wa watanzania. Viongozi hao wa kidini wamesema jambo la kutembelea hifadhi za kitaifa ni moja ya shughuli muhimu ya kuutazama ukuu wa Mungu.
Mwenyekiti wa Shirika la TANUA nchini Ndg Enock Bujuli Akifafanua kuhusu Shirika la TANUA na chombo cha kusimamia utalii wa ndani nchini |
Ø Wanyama
Ø Milima na mabonde yenye mandhari nzuri
Ø Uwepo wa hot spring
Ø Mabwawa na misitu yenye kuvutia
Ø Aina 175 za ndege wenye kuvutia
Ø Mto kagera
Ø Boma wazi Unganishi kwa nchi Tatu yaani Tanzania, Uganda na Rwanda.
Mgeni Rasmi Bi Upendo Massawe Akitangaza vivutio vilivyopo katika hifadhi ya Taifa Ibanda-kyerwa |
Mkurugenzi wa kampuni ya HLUCK KOMBUCHA INVERSTMENT Ndg Hamisi H Jumanne aliwaomba watanzania kupenda kutumia na kusapoti bidhaa za ndani ikiwemo kinywaji cha Kombucha wine kilichotengenezwa kwa bidhaa ghafi za ndani.
Mkurugenzi wa kampuni ya HLUCK KOMBUCHA INVERSTMENT Ndg Hamisi H Jumanne Akitambulisha Fursa katika sekta ya utalii kupitia vinywaji vya Kombucha Wine |
Naye ndugu Erasto Bwenge Amewasihi wakulima kuendelea kuzalisha na kutumia bidhaa za ndani ikiwemo kinywaji cha Banana wine kinachotengenezwa kwa ndizi zinazolimwa mkoani Kagera hususani wilayani Karagwe.
TANUA walifanikiwa pia Kuendesha semina zenye kulenga kuhamasisha ulipaji wa KODI kwa watanzania kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi. Shughuli hii ilianza mwanzoni mwa mwezi wa kwanza huku ikijumuhisha wilaya 11 za Tanzania bara.
Kuhusu safari ya Ibanda January 01-2021
Kwa mujibu wa mratibu wa safari ya utalii wa ndani katika hifadhi ya Taifa ya Ibanda, safari ya kitalii inatarajiwa kufanyika January mosi mwaka 2021.
Safari hii itahusisha Wilaya mama za mkoa wa Kagera ikiwemo Karagwe, Bukoba, Missenyi, Muleba, Biharamulo, Kyerwa na Ngara pamoja na wilaya jirani yaChato mkoani Geita.
Kamati ya kuhamasisha utalii wa ndani chini ya mwavuli wa TANUA ,imetoa shukrani kwa wawezeshaji wa shughuli hiyo ikiwemo Bank ya NMB, Hlucky Kombucha Inv, Banana wine, wajumbe Pamoja na wageni waalikwa wa kiwemo wakuu wa mashule na wadau Mbalimbali.
Picha ya pamoja ya Kamati kuu bodi ya utalii pamoja na wageni waalikwa |
Wajumbe wa kamati kuu bodi ya Utalii chini ya TANUA na wageni waalikwa katika Picha ya pamoja |
USICHOKIJUA KUHUSU TANUA
Shirika la TANUA limekua nuru iwakayo katika kutia chachu ya maendeleo na kuibua shughuli mbalimbali zenye kuongeza pato la taifa na kuinua uchumi wa watanzania kwa ujumla.
TANUA ilifanikiwa kupeleka watalii wa ndani wapatao 100 katika Mbuga za wanyama Chato-Burigi ikiwa ni safari ya kwanza katika Mbuga hizo kuwa na wazawa wengi wenye lengo la kushuhudia utajiri wa nchi yao na kuchangia pato la taifa. Safari hiyo ilifanyika mwishoni mwa mwezi wa nane mwaka huu 2020 huku wakipata kuungwa mkono na Viongozi mbali mbali wa kiserikali, wakisindikizwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Kagera Prof; Kamzola.
TANUA pia mwaka 2016 Walifanikisha Matembezi ya kuhamasisha Amani nchini. Matembezi hayo yalianzia Mkoa wa Dar es salaam Mpaka Mkoani Mwanza, alieleza Mwenyekiti wa shirika hilo Ndg Enock Bujuli
Na BakalemwaTZ (EDUSPORTSTZ)
Social Plugin