Na Samirah Yusuph
Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu imepewa jukumu la kuhakikisha kuwa Asilimia 97 ya kura za mgombea nafasi ya Rais kwa tiketi ya chama hicho zinapatIkana kutoka katika mkoa huu.
Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu imepewa jukumu la kuhakikisha kuwa Asilimia 97 ya kura za mgombea nafasi ya Rais kwa tiketi ya chama hicho zinapatIkana kutoka katika mkoa huu.
Jukumu hilo limetolewa na katibu wa mkoa wa Simiyu Haula Kachwamba alipokuwa akizungumza na vijana hao baada ya matembezi ya hamasa kwa ajili ya maandalizi ya kumpokea mgombea wa ngazi ya Rais mkoani hapo tarehe nne mwezi wa nane 2020.
"Asilimia kubwa ya wapiga kura wetu ni vijana hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha vijana wanatumika kura ili kuweza kufikia lengo la asilimia 97 ya kura za mheshimiwa rais " alisema Haula
Akiweka mkazo wa namna ambavyo wamejiandaa katika kutafuta kura hizo mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Bariadi Mayiku, alisema kuwa wao wamejipanga katika kuhakikisha kura hizo zinapatikana.
"Huu ni ujumbe kwa vyama vya upinzani na wajue kuwa tumejipanga na tunaomba wajitokeze kwa wingi ili tumwambie mheshimiwa raisi kuwa asilimia 100 ataipata Simiyu," Alisema Mayiku.
"Kiupekee ni washukuru kwa kushiriki matembezi haya ambayo yamefikisha taarifa kwa wapinzani sisi ni kina nani na ninawaomba kesho pia mjitokeze kwa ajili ya kumpokea mgombea wetu kiti cha rais," alisema Rucy John Sabu Mbunge mteule vijana mkoa wa Simiyu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya vijana wa ccm mkoa wa simiyu Lumeni mathias alisema kuwa matembezi hayo yalikuwa na zaidi ya vijana 300 ambayo yalilenga kuwataarifu vijana na wananchi kwa ujumla kuwa kesho kuna ujio wa mgombea wa nafasi ya Rais katika mkoa huo.
Social Plugin