Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation Neema
Lugangira akizungumza wakati wa semina hiyo |
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation Rehema Maro akizungumza wakati wa semina hiyo |
KATIBU wa UWT Mkoa wa Tanga akizungumza wakati wa semina hiyo Sophia Nkupe |
MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Husna Sekiboko |
Sehemu ya washiriki kwenye semina hiyo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema kwamba kamwe hatawajibu wanaomtukana kwenye majukwaa badala yake ataeleza namna nitakavyoweza kuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wakati akipewa ridhaa ya kuwaongoza.
Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema hayo leo wakati semina hiyo itasaidia kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi semina hiyo imeandaliwa na Shirika la Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) ikiratibiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation .
Alisema kwamba atakachokifanya wakati akiendesha kampeni zake za kuwania Ubunge Jimbo hilo atajikita kwenye kueleza namna atakavyosaidia wananchi kuweza kujikwamua kimaendeleo kwa kuona namna ya kushirikiana nao katika kufikia mafanikio.
“Niseme tu kwamba nitakapokuwa kwenye kampeni sitatumia jukwaa kuwajibu ambao wananitukana badala yake nitajikita kwenye kutangaza maendeleo makubwa na mipango ambayo nitawafanyia wananchi wa Jimbo la Tanga lakini pia niwashukuru wajumbe wa UWT kwa sapoti kubwa kwangu”Alisema
Hata hivyo aliwaomba wanawake wanaowania uongozi kwenye nafasi mbalimbali wasiwe mawakala wa kuwatukana watu ikiwemo kuwadhalilisha wanawake wenzao na ukisikia neno limesemwa mwananke unakuwa wa kwanza kulishikia bango hiyo sio sawa hakikisheni mnabadilika.
Ummy aliwataka pia kuhakikisha hawawi mawakala wa kusambaza mambo ya ovyo yanayodhalilisha utu na haki ya wanawake kwa sababu wao ndio walezi wa familia na ndio watapambanaji ambao wanalea familia hivyo watambue wana umuhimu mkubwa kwenye jamii
“Ndugu zangu tusifanye kampeni za matusi za kudhalilisha wanawake wenzetu kwenye majukwa lakini niwaambie kwamba wakati wa kampeni zangu hawatanisikia nikiwajibu ambao wananitukana badala yake nitajikita kwenye kutangaza namna nitakavyoleta maendeleo”Alisema Ummy Mwalimu.
Hata hivyo aliwataka wanawake kuhakikisha wanasaidiana, kuacha kuoneana wivu na choyo badala yake washirikiane katika kujiletea maendeleo ambayo yatawasaidia kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii ambazo zinawazunguka.
Ummy aliwaomba wakati mwengine kuipeleka semina hiyo katika mikoa mingine wanawake kuwa mstari wa mbele kupigania vipaumbele vya wanawake katika afya ya mama na mtoto, elimu kwa watoto wa kike kwa lengo la kuweza kuwakomboa
Awali akizungumza wakati wa semina hiyo, Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira amesema wamejikita kutoa elimu kwenye masuala ya lishe na kuhamamisha kilimo lishe.
Alisema kwamba mwaka juzi walianza mchakato maalumu wa kisera kuhakikisha agenda hiyo inaingia kikamilifu kwenye ilani ya uchaguzi mafanikio ilani ya uchaguzi ya CCM 2020/2025 agenda ya lishe imeingia kikamilifu kwani imekuwa kati ya vipaumbele vikubwa ya CCM.
Neema alisema kwa sababu watoto wanapokuwa na lishe duni hiyo ndio nguvu kazi ya kesho ili Taifa lolote likuwa lazima kuwepo na nguvu kazi thabiti ya kiuchumi
Hata hivyo alisema aganeda ya lishe imepata nafasi yake maalumu kwenye ilani ya CCM ya Mwaka 2020/2025 kati ya malengo ni kushuha hali ya udumuvu hadi kufikia kiwango cha asilimia 24 ndani ya miaka mitano.
Social Plugin