Mudiri wa Taasisi
ya Shamsul Maarifa Islamiyyah Shehe Samiri Hemed kulia akipimwa kabla ya kuanza zoezi la uchangiaji wa damu kwa ajili ya kuongeza
damu kwenye benki ya damu salama katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Tanga Bombo.
***
TAASISI ya Shamsul Maarifa Islamiyyah ya Jijini Tanga
imeendesha zoezi la utoaji na uchangiaji wa damu kwa ajili ya kuongeza
damu kwenye benki ya damu salama katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Tanga Bombo.
Uchangiaji huo ulifanyika kwenye taasisi hiyo ikiwa ni
kuelekea maadhimisho ya Taasisi hiyo tokea ilipoanzishwa miaka 20
iliyopita ambayo hufanyika kila mwaka ikiwamo ufunguzi wa madarasa
mapya.
Akizingumza na waandishi wa habari Mudiri wa Taasisi
ya Shamsul Maarifa Islamiyyah Shehe Samiri Hemed alisema huo ni mwaka wa
20 tokea walivyoanza madrasa hiyo mwaka 2000.
Alisema kwamba wapo kwenye kumbukumbu yao ya kila mwaka
kusherekea kuadhimisha elimu na miaka 20 ya Shamsi Maarifa ambapo
wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali wa kijamii.
Shehe Samir alisema moja ya shughuli ambayo wanaifanya
kuelekea maadhimisho hayo ni zoezi la utoaji na uchangiaji wa damu kwa
ajili ya kuongeza damu kwenye benki ya damu.
Alisema hilo ni moja ya mafunzo ya waislamu kusaidiana na
kumsaidia mwengine akiwa kwenye hali ya uzima na ugonjwa kama
wanavyofahamu damu kuwepo kwenye benki ya damu ni moja katikati vitu
muhimu vinavyohitajika kwa ajili ya afya ya wanadamu kuisaidia jamii.
“Kwani mtu anaweza kwenda hospitali kwa hali ya sasa hata
akienda na mchangiaji wa damu wa kumtolea kama benki ya damu hakuna kitu
damu hiyo hawezi kuongezewa mgonjwa hivyo tupo kuisaidia jamii
tunafanya zoezi hilo mara kwa mara kuchangia damu inapohitajika”,alisema.
Aidha alisema safari hii wameifanya iwe rasmi kusherehekea
miaka 2o ya shamsi maarifa itakayokwenda samabamba na ufunguzi wa
madarasa mapya 10 waliyoyapata kupitia ufadhili wa Taasisi inayoitwa
Fildaus.
Hata hivyo alisema majengo hayo yatatumika kusomea hivyo
watashiriki kufanya ufunguzi wa madarasa hayo na wamealika wageni kutoka
ndani ya nchi na nje ya nchi ambao watashiriki kwenye maadhimoisho hao
ya kuadhimisha miaka 20.
Awali akizungumza katika halfa hiyo Naibu Katibu Mkuu wa
Shamsul Maarifa Islamiyyah Hamisi Haruna Mbolele alitoa wito kwa jamii
kushirikiana na Taasisi ya Jai katika masuala hayo huku akiziomba
taasisi nyengine ikiwemo Shamsul, Zaharau na Maawal waweze kujumuika
kwenye jambo hilo.
Alisema kilele cha maadhimisho ya Taasisi hiyo kitafanyika
Jumapili wiki hii huku kwa siku zinazoendelea itaanza Septemba 4 huku
akiendelea kutoa wito kwa taasisi nyengine ambazo zinaweza kujitokeza
kuchangia damu na watu mbalimbali wafike.