Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TBS : UPATIKANAJI WA MAFUTA NCHINI NI TANI LAKI 2 KWA MWAKA



Takwimu zinaonesha mahitaji ya mafuta ya kula nchini ni tani laki nne kwa mwaka wakati uzalishaji unaofanyika ni tani laki mbili kwa sasa hivyo Serikali imeamua kutoa mafunzo kwa wazalishaji wa mafuta ya kula ili kuongeza wingi wa mafuta hayo kwa mahitaji ya nchi.

Hayo yamesemwa leo na Meneja wa Utafiti na Mafunzo kutoka Shirika la Viwango Tanzania TBS, Bw.Hamis Sudi wakati wa mafunzo kwa wazalishaji wa mafuta ya kula Mkoani Tabora.

Sudi amesema kuwa utoaji wa mafunzo kwa wazalishaji hao utaongeza nguvu kwa uzalishaji wa mafuta hayo kwasababu mngin yankuwa yanaota katika mnyororo mzima wa uzalishaji.

"Tunatumia fursa hii kuwaelezea majukumu ya TBS ikiwa na pamoja na yale ambayo yalikuwa yanafanywa na TFDA majukumu hayo ni pamoja usajili wa vyakula na vipodozi lakini na majengo,wale watu wa mabucha,migahawa,supemarket na wale wenye maghala kwamba ni namna gani shuguli zile zinazofanywa na TBS, na kimsingi ufanisi wa kazi bado upo",amesema Sudi.

Amesema kwenye mafunzo hayo wanawashirikisha wataalamu kutoka SIDO pamoja na mwakilishi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara ia wanatumia wenyeji wao kufanikisha zoezi hilo.

Pamoja na hayo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kueleza changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za kibiashara ili waweze kupata majawabu na kuweza kuzalisha bidhaa iliyobora na kuweza kupata masoko makubwa na uzalishaji kuongezeka.

Mpaka sasa wameshafikiwa wadau zaidi ya 680 katika mikoa ya Singida na Tabora.
Meneja wa Mafunzo na Utafiti wa TBS Bw. Hamisi Sudi, akitoa elimu ya vifungashio bora kwa wadau wa mafuta ya kula katika Manispaa ya Tabora.Wazalishaji wa mafuta ya kula wakifuatilia mafunzo katika Manispaa ya Tabora

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com