Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TRUMP AAPA KUJIBU SHAMBULIO LA IRAN MARA 1,000 ZAIDI

Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kwamba shambulio lolote litakalofanywa na Iran litajibiwa mara 1,000 kwa ukubwa, baada ya ripoti kuwa Iran inapanga kulipiza kisasi baada ya kuuliwa jenerali wa ngazi ya juu Qasem Soleimani. 

Ripoti ya vyombo vya habari nchini Marekani, zimenukuu maafisa ambao hawakutajwa majina, wakisema kuwa mpango unaodaiwa kupangwa na Iran wa kumuua balozi wa Marekani nchini Afrika kusini ulipangwa kabla ya uchaguzi wa rais mwezi Novemba.

 Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, Iran inaweza kuwa inapanga mauaji hayo, ama mashambulizi mengine, dhidi ya Marekani kwa kulipiza kisasi kwa kuuliwa kwa jenerali wa Iran Soleimani, Trump aliandika katika ukurasa wa Twitter. 

Amesema shambulio lolote litakalofanywa na Iran, kwa njia yoyote ile, dhidi ya Marekani litajibiwa kwa shambulio kubwa zaidi ambalo litakuwa mara 1,000 zaidi kwa ukubwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com