Wadukuzi kutoka Urusi, China na Iran wanajaribu kuingilia Uchaguzi wa urais nchini Marekani utakaofanyika tarehe tatu mwezi Novemba kwa mujibu wa kampuni ya teknolojia ya Microsoft.
Kulingana na Microsoft, wadukuzi hao walilenga wafanyakazi pamoja na mashirika yanayoendesha kampeni za rais Donald Trump na mpinzani wake Joe Biden katika mashambulizi ya hivi karibuni.
Microsoft inasema ilifanikiwa kusitisha mashambulizi kutoka kundi la wadukuzi la Stronium la Urusi, Zirconium la China Phosphorus la Iran yaliolenga akaunti za watu binafsi na mashirika yanayohusika na kampeni ya rais Trump na mpinzani wake Biden.
Haya yanajiri wakati, idara ya usalama wa nchi, Marekani, ikiituhumu Urusi kwa kujaribu kuondoa imani ya wapiga kuru katika mfumo wa uchaguzi wa Marekani wakati huu nchi hiyo ikielekea uchaguzi wa mwzei Novemba
Mwezi Agosti, kituo cha ujasusi na usalama wa kitaifa ulisema kuwa Urusi inafanya kazi dhidi ya mgombea wa urais Joe Biden, huku ikimpendelea rais Trump kama ilivyofanya katika uchaguzi wa 2016.
Credit: RFI
Social Plugin