UMMY KUANZISHA UJENZI WA HOSTELI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI JIJINI TANGA

 

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa Kata ya Mzizima Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akimnadi mgombea udiwani wa Kata ya Mzizima Fredrick Chiluba wakati wa mkutano wake wa kampeni
Mgombea udiwani wa Kata ya Mzizima Fredrick Chiluba kushoto akimuombea kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia wakati wa mkutano wake wa kampeni
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na mgombea udiwani wa kata ya Mzizima Fredrick Chiluba wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba
Msanii Kassim Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo
Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia mkutano huo

Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia mkutano huo

Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia mkutano huo

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema akichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo atajitahidi kuanzisha ujenzi wa hosteli kwa wanafunzi wanaosoma shule za sekondari wanaokaa mbali ili kuwawezesha kusoma bila uwepo wa vikwazo.

Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule za Sekondari kukaa mbali na maeneo ya shule hali inayopelekea kushindwa kufika  kwa wakati kutokana na changamoto ya usafiri.

Ummy aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mzizima katika uwanja wa Gogovivu kwenye mkutano wake wa kampeni ambapo alisema suala hilo litakuwa mwarobaini wa kuwaepusha wanafunzi kutokufika shuleni.

 “Ninaamini ujenzi wa Hostel utasaidia kupunguza changamoto ambazo zinawakabili wanafunzi wanaosoma shule za mbali kutokana na kukosekana kwa usafiri kwa baadhi ya maeneo wanayokwenda”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba ataendelea pia kushirikiana nao  kujenga miundombinu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari.

“Ninafahamu shule za msingi Mafuriko,amboni,rubawa na mleni kuna maadhibi miomdnboni sio mizuri na madarasa hayatoshi,ninawaomba sana ..mchango wangu niliiutoa kabla sijawa mbunge niaminini niweze kushirikiana nanyi kuboresha elimu hasa miundombinu na kutafuta madawati kwa ajili ya wanafunzi”Alisema Ummy

“Lakini pia sijaisahau shule ya sekondari Kiomoni nimewekeza ujenzi wa madarasa mawili ninawaomba sana mnichague ili tuweze kuiboresha zaidi”Alisema

Hata hivyo alisema pia atalazimika kubadilisha jina la shule ya sekondari Kiomoni kwa sababu ni ya shule ya kata ya Mzizima hivyo watabadilisha jina liweze kuwa shule ya sekondari Mzizima.

“Niaminini tuweze kutatua changamoto za wanafunzi wa Rubawa,Mleni  ambao wanakwenda mpaka sekondari ya kiomoni kwa  usafiri wenye changamoto na kupelekea kushindwa kufika shuleni kwa wakati”Alisema 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post