Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo aliwataka wananchi kumchagua Ummy Mwalimu |
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati amkifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima |
MSANII wa Mziki wa Bongofleva Jijini Tanga Mwandey akitumbuiza kwenye mkutano huo wa kampeni
Msanii wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza kwenye kampeni hizo |
Msanii wa Mziki wa Bongofleva Mchina Mweusi akitumbuiza kwenye mkutano huo |
Msanii wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza kwenye kampeni hizo |
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Ummy Mwalimu wakati akinadi sera zake
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akipandisha bendera ya CCM mara baada ya kuzindua shina la Wakereketwa Wajasiriamali Womens Group
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amehaidi iwapo akichaguliwa atawawezesha
kiuchumii wakina mama wajasiriamali wadogo wadogo na watu wenye ulemavu kupatiwa
mikopo isiyo na riba ili waweze kufanya shughuli zao za kuzalisha mali.
Huku
akiwahaidi pia vijana nao pia watapatiwa mikop na
vitendea kazi ikiwemo pikipiki alimaarufu bodaboda ili waweze kufanya biashara
za bodaboda bila kulipa fedha nyingi ambazo wanapaswa kulipa.
Ummy
ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto alitoa
ahadi hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mabawa Jijini Tanga ambapo
alisema atafanya kazi usiku na mchana ili kuweza kutatua changamoto za
wananchi.
Alisema
dhana hizo ni kuwapatia pikipiki ili wafanya biashara ya bodaboda ambayo
itawasaidi waweze kujiingizia kipato ambacho kitawasaidia kujikwamua
kimaendeleo na hatimaye kukuza kipato chao.
“Ndugu
zangu wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo wadogo,watu wenye ulemavu tuwapa
mikopo muweza kuongeza kipato chenu na hii itawasaidia kuinuka kiuchumi kwenye
biashara zenu”,alisema Ummy Mwalimu.
Aliwataka
wampigia kura za ndio ili wamuweze kuwa mbunge wa Jimbo hilo ili aweze
kuhakikisha anawatumikia wananchi hao ili waweze kupiga hatua kubwa ya
kimaendeleo.
“Lakini
pia niwaombe tume kura nyingi za ndio Rais Dkt John Magufuli aendele kwani kazi
yake kwenye Jiji la Tanga inaonekana kwenye sekta ya elimu amewezesha utoaji wa
elimu bure,ujenzi wa madarasa nyumba vya maabara”,alisema.
Hata
hivyo alisema pia kazi ya Rais Dkt Magufuli kwenye sekta ya afya kwenye kata ya
mabawa imeonakana kwani hamkuwa na kituo cha fya lakini leo kumejenga majengo ya upasuaji wodi za watoto
na wakina mama.
“Kwa
heshima na taadhima nawaomba msifanya makosa mpeni kura za ndio Rais Dkt John Magufuli
kwenye uchaguzi mkuu mwezi Octoba mwaka huu lakini pia naombeni kura zenu zote
za ndio niweze kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kwenye Jiji la Tanga”,alisema.
Hata
hivyo alisema kwamba hakuna mgombea Urais ambaye anaweza kufikia kazi zilizofanywa
na Rais Dkt Magufuli hata kwa asilimia 1 .