UPATIKANAJI UMEME KUIMARIKA BAADA YA UJENZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME CHA ZUZU KUKAMILIKA

Wakurugenzi wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) wakimsikiliza Kaimu Meneja wa Kituo cha Zuzu,Said Runyilija walipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dkt.Alexander Kyaruzi (katikati) akiongoza wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO walipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.

Baadhi ya Mitambo inayofanya kazi katika kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.

Sehemu ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dkt.Alexander Kyaruzi (katikati) akiwa na wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO wakimsikiliza Mratibu wa Mradi wa kituo cha kupoza umeme Zuzu, Mhandisi Peter Kigadye walipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho kilichopo jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dkt.Alexander Kyaruzi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho kilichopo jijini Dodoma.

Mratibu wa Mradi wa kituo cha kupoza umeme Zuzu, Mhandisi Peter Kigadye,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dkt.Alexander Kyaruzi akiongoza wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO kutembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho kilichopo jijini Dodoma.

............................................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mwenyekiti BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), Mhandisi Alexender Kyaruzi amesema kuwa upatikanaji wa umeme utaimarika baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu jijini hapa ambacho kitazalisha umeme wa Megawati 250.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Mhandisi Kyaruzi wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua ujenzi huo iliyofanywa na bodi hiyo.

Aidha Mhandisi Kyaruzi ameeleza kuwa kwasasa kituo kinazalisha Megawati 48 ambazo haziwezi kutosheleza kutokana na ongezeko la watu kwa mkoa huo.

“baada ya kukamilika kwa kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 250 ambapo ukizijumlisha na Megawati 48, kitakuwa na takriban Megawati 300 ambao utakuwa umeme mwingi sana”ameeleza Mhandisi Kyaruzi.

Mhandisi Kyaruzi amesema kuwa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika Septemba 15 mwaka huu na Septemba 30 wataanza kufanya majaribio ya uzalishaji wa umeme hali itakayoongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa mkoa wa Dodoma.

"Kituo hiki kikikamilika tunaamini kabisa tutakuwa na Umeme mwingi na wa uhakika mana kwa sasa zinazalishwa Megawati 48, lakini kikikamilika kitazalisha Megawati 250, huu ni Umeme mwingi sana,"amesisitiza.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa kituo hicho, Mhandisi Peter Kigadye, ameeleza kuwa kituo hicho kitakuwa kikipokea umeme kilovati 400 na kupooza kwenda 220 hadi 33.

Pia Kigadye ameweka wazi kuwa mwakani wanatarajia kujenga laini 8 imara na za uhakika ambazo zitawezesha kutawanywa umeme katika mkoa mzima wa Dodoma na viunga vyake.

“ Baada ya kukamilika kwa kituo hiki tunatarajia kujenga vituo vya umeme(substation), Wilaya ya Kongwa na mji wa serikali vyote vitakuwa na uwezo wa kuongeza usambazaji wa umeme wa uhakika”, amesema Kigadye

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post