Watumishi wa umma waliochukua fomu kugombea majimbo mbalimbali na kushindwa wamerejea rasmi maeneo yao ya kazi leo Septemba 1, 2020.
Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Dkt. Francis Michael ameamuru watumishi hao wa umma kuanza kulipwa mishahara yao kuanzia mwezi huu.
Aidha, Dkt. Michael amefafanua kuwa msaidizi wa kiongozi yeyote wakiwemo mawaziri hawapaswi kuendelea na kazi ikiwa mkuu wake anagombea na endapo atataka kushiriki pamoja naye ni lazima aombe likizo isiyo na malipo.
Kwa kuongezea, Michael ameyataja badhi ya makundi yasiyoruhusiwa kujiunga na chama chochote cha siasa kuwa ni watumishi wa majeshi yote, ofisi ya mwanasheria mkuu, watumishi wa ofisi ya NEC, ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, ofisi ya Bunge, majaji, mahakimu, mawakili wa Serikali, Idara ya Usalama wa Taifa na Idara ya Uhamiaji.