KATIBU wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Khatibu Kilenga akizungumza jambo wakati wa mkutano huo |
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kikao hicho kushoto ni Mkurugenzi wa
Asasi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga Fortunata Manyeresa na wa pili kulia ni Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia kundi Asasi
za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara (CCM) Neema Lugangira
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyataka mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali nchini kuzingatia uwazi na uwajibikaji kwenye shughuli
zao ikiwemo fedha hasa wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu.
Ummy
ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM)aliyasema
hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa asasi za kiraia (NGOs) zinazofanya
kazi Halmashauri ya Jiji la Tanga na mkoa wa Tanga ambapo kikao hicho
kimehudhuriwa na wadau mbalimbali.
Alisema
hategemei kuona shirika lisilokuwa la kiserikali linapata fedha za kwa ajili ya
kuchochea mpasuko na masuala yatakayoleta mfarakano kati ya watanzania kubwa
waendelee kuheshimu sheria, kanuni zinazosimamia mashirika hayo.
Aidha
alisema lazima wafanye kazi kwa malengo waliyoyaomba na sio kujiingiza kwenye
masuala mengine yatakayohatarisha umoja na mshikamano kwenye nchi ambayo ni
tunu kubwa.
Waziri
Ummy aliyataka pia mashirika hayo kuhakikisha rasilimali fedha wanazozipata ambazo
wanaziomba kwa jina la watanzania kuzitumia kikamilifu kwa ajili ya wananachi
wanaoombea fedha hizozna sio kwa maslahi yao binafsi.
“Lakini
kubwa amesisitiza uwazi na uwajibukaji kwa asasi za kiraia kwa wananchi na serikali
na ndio maana mwaka 2019 tulitoa kanuni mpya za mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali ambayo yanazitaka kila asasi inayopokea fedha inayozidi milioni 20
kuhakikisha inatoa taarifa kila baada ya miwezi mitatu kwa Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii namna zitakavyotumika na matokeo yanayotarajiwa”Alisema.
Awali
akizungumza wakati wa mkutano huo Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia kundi Asasi
za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara (CCM) Neema Lugangira amewaambia viongozi wa
asasi hizo mkoani Tanga huku akieleza kazi yake kubwa ni kuwa kiunganishi kati
ya NGOs, Bunge, Serikali, CCM na wafadhili ili waweze kupata mafanikio.
Alisema
dhamira ya kukutana na viongozi wa NGOs za Mkoa wa Tanga ni dhumuni kubwa
likiwa ni kumwezesha kupata uelewa wa changamoto zao ili aweze kuandaa
vipaumbele vyake.
Alisema
kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatambua kazi kubwa inayofanywa na Asasi
hizo hapa nchini na ndio maana katika vipaumbele vikuu vya CCM kwenye ilani ya
mwaka 2025.
Neema
aliwathibitishia viongozi wa (NGOs) mkoa wa Tanga kwamba CCM inatambua kazi kubwa
inayofanywa na Asasi hizo nchini na ndio maana katika vipaumbele vyake vikuu
kwenye ilani a 2020 -2025.
“Kuchukua
hatua madhubuti za kujenga mazingira wenzeshi kwa asasi za kiraia, kidini na
vyombo vya habari kulinda kustawi ili kuchangia maendeleo ya Taifa”Alisema
Neema.
Aidha
alisema maendeleo hayana chama wala dini hivyo kupitia nafasi hiyo atahakikisha
anawaunganisha ili kuweza kuwa chachu kubwa ya maendeleo kwao.
“Lakini
wana Tanga mtambue kwamba nyie ni asasi za kwanza za kiraia ambao tunakutana
nanyi tokea nimetangazwa Agosti 20 mwaka huu naamini wadau wa asasi za kiraia
hatuna mambo ya vyama.
“Ila
mtanisamehe siku ya leo wakati narejea ilani ya CCM muone namna gani ilani
inatambua NGOs kama wadau muhimu ambao wanashirikiana na serikali katika
kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii yetu”Alisema
Social Plugin