Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YANGA YABADILI KAMBI, ICHEKI KAMBI YAO MPYA KAMA ULAYA

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Hii sasa sifa!!! Kutokea Mikocheni hadi Kimbiji, kikosi cha timu ya Yanga kwa sasa wanatarajiwa kuhamia Kimbiji katika kambi mpya wakitokea Mikocheni.

Hatua hiyo inakuja baada ya mdhamini wao GSM kuamua kuwabadilishia kambi na kuwapeleka nje ya mji ili kupata muda zaidi wa kujifua na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kambi hiyo mpya ya Yanga ina mahitaji yote ikiwemo Uwanja wa mazoezi wa mpira wa miguu, Kikapu na michezo mingine.

Mabadiliko hayo yanafanyika muda mfupi kabla ya kuanza kwa Ligi msimu 2020/21 siku ya Jumapili wakitokea katika kilele cha siku ya Mwananchi.

Yanga ilifanya kilele cha siku ya Mwananchi siku ya Jumapili Agosti 30, na kuweka historia ya kujaza uwanja pamoja na kuwa tamasha lililovutia na kufana likonogeshwa na Msanii Harmonize huku wakicheza Mchezo wa Kirafiki dhidhi Agle Noir.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com