AIRO AMNADI CHEGE KIJIJINI KWAO NYANDUGA... CHEGE AMUOMBA AIRO APUUZE WACHONGANISHI


Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Rorya mkoani Mara Lameck Airo (kulia) akicheza na Kikundi cha kwaya kutoka kijiji cha Nyanduga 

Na Dinna Maningo,Rorya
Aliyekuwa mbunge jimbo la Rorya mkoani Mara kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Lameck Airo amewaomba wananchi wa kijiji cha Nyanduga kata ya Koryo kumpigia kura mgombea ubunge Jafari Chege.

Airo aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa wananchi uliofanyika kijiji cha Nyanduga wakati akimnadi Chege ambapo alisema kuwa Chege ndiyo anafaa kuwa mbunge Rorya na endapo wakimchagua atayaendeleza yale ambayo hakuyatekeleza wakati wa ubunge wake.

"Wananchi naomba mpigieni kura Chege huyu ni mwana CCM tusichague mtu kwa sababu ya ukoo anaotoka, wakati wa uchaguzi wa ubunge wangu Tarafa ya Suba ndiyo waliongoza kunipa kura nyingi ambayo ndiyo Tarafa anayotoka mgombea wetu Chege,kata ya Koryo ndiyo mliongoza kwa kura nyingi kunipigia naomba na Chege mpeni kura nyingi ili iwekwe kumbukumbu kuwa Koryo mliongoza kwa kura nyingi", alisema Airo.

Airo aliwaambia wananchi kuwa kura za maoni zisiwagawe vipande vipande na aliahidi kuwa hata kama amestaafu Ubunge ataendelea kushirikiana na Chege katika maendeleo ya Rorya.

Aliwaomba wananchi kumchagua Rais Magufuli kwa kuwa amefanya maendeleo na anawajali wanyonge,lakini pia kumpigia kura mgombea udiwani kata ya Koryo Nelson Simba aliyekuwa mkuu wa shule ya msingi Utegi na Mratibu elimu Kata na kisha kustaafu utumishi.

"Tumeziona kazi zake alipokuwa mwalimu ni mtu wa kijituma,anajishusha kiongozi mzuri ni yule anaejishusha,mambo ya siasa na kura za maoni zisitugawe vipande vipande naomba wananchi msije kuniangusha ipigieni CCM ishinde kwa kishindo", alisema Airo.

Mgombea ubunge wa jimbo hilo Jafari Chege aliwaomba wananchi kumpigia kura huku akimpongeza Airo kwa maendeleo aliyoyafanya licha ya kuwa na elimu ya darasa la saba na aliahidi kuendeleza pale alipoishia.

"Airo nakuomba wapuuze wachonganishi na wanaotugawa kama kuna Wasuba wanakulalamikia kwenye mitandao ya kijamii wacha walalamike sisi tunatafuta mbunge wa Rorya na siyo wa koo,nimejifunza vitu vingi kupitia Airo kumbe bila kujali elimu uliyonayo unaweza kufanya mengi.

"Airo amefanya kazi kubwa ukienda Tarafa ya Suba wanamkumbuka hata baba yangu anamzungumza sana na amekuwa mpiga kura wake,katika uongozi wake kapambana vijiji 74 vimepata umeme ameniachia vijiji 13 na mimi ntahakikisha namalizia na umeme utakwenda hadi kwenye vitongoji",alisema Chege.

Chege alisema kuwa kazi yake ni kutekeleza Ilani ya CCM na yaliyofanywa na Airo na kwamba wakimpatia kura atahakikisha yale yaliyosalia kwa Airo anayatekeleza ikiwemo changamoto ya daraja linalounganisha watu wa kata ya Mirare na Koryo, kero ya maji na pale atakapokwama Airo atamuunga mkono.

Akizungumzia suala la wizi wa mifugo alisema"Kuna wanaosema kwamba mkimchagua Chege wizi utazidi,kwa kuniangalia mimi naweza kuwa mwizi wa ng'ombe! nipeni kura nitahakikisha nadhibiti wizi kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya na Airo atanifundisha mbinu zake maana alifanikiwa sana kudhibiti wizi",alisema Chege.

Chege alimuombea kura Rais Magufuli na mgombea Udiwani huku akisisitiza kuwa Airo alifanikiwa katika ubunge wake kwa kuwa alikuwa mbunge wa CCM na Rais Magufuli ni CCM na kata ya Koryo iliongozwa na diwani wa CCM.


Godwin Owawa aliyekuwa mtiania wa ubunge jimbo la Kawe -Dar es Salaam aliwaomba wananchi kutowasikiliza watu wanaozungumza uongo na waichague CCM huku Godfrey Obonyo akipinga ubaguzi wa koo na ukabila.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Rorya mkoani Mara Lameck Airo (kulia) akicheza na Kikundi cha kwaya kutoka kijiji cha Nyanduga
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Rorya mkoani Mara Lameck Airo (kulia) akicheza na Kikundi cha kwaya kutoka kijiji cha Nyanduga
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Rorya mkoani Mara Lameck Airo (kulia) akicheza na Kikundi cha kwaya kutoka kijiji cha Nyanduga

Aliyeketi mbele mwenye kofia ya kijani ni Jafari Chege mgombea ubunge jimbo la Rorya
Lameck Airo akizungumza na wananchi wa Nyanduga na kumuombea kura Jafari Chege.
Mgombea Ubunge Jimbo la Rorya Jafari Chege akiomba kura kwa wananchi.
Walioketi mbele kushoto ni Jafari Chege mgombea ubunge jimbo la Rorya na Lameck Airo aliyekuwa mbunge jimbo la Rorya.

Wananchi wa kijiji cha Nyanduga wakiwa kwenye mkutano wa kumsikiliza mgombea ubunge Jafari Chege wa CCM
Vikundi vya burudani kutoka kijiji cha Nyanduga vikitoa burudani

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post