Waendesha baiskeli wakianza mashindano kutoka Shinyanga Mjini kuelekea Isaka (KM 150)
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi imeendesha Mashindano ya Mbio za Baiskeli ‘CRDB SHINYANGA CYCLING RALLY’ na kuendesha zoezi la Uchangiaji Damu Salama ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 21 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Maadhimisho hayo yalitawaliwa na mbio za Baiskeli yaliyoleta burudani ya aina yake kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga na maeneo Jirani yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB ikishirikiana na wadau mbalimbali yakiongoza na kauli mbiu ya ‘Shinyanga Yetu, Damu Yetu’ yamefanyika leo Jumatano Oktoba 14,2020 katika Uwanja wa CCM Kambarage na barabara ya Shinyanga kwenda Kahama ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.
Waendesha baiskeli walionesha umahiri wao wa kuendesha baiskeli kwa kasi na umakini mkubwa katika mashindano ya wanaume masafa marefu kwa umbali wa Kilomita 150 kutoka Shinyanga kwenda Isaka, huku kundi jingine likiendesha baiskeli kwa umbali wa kilomita 80 kutoka Shinyanga Mjini kwenda Kituli huku Wazee kundi la wanaume wakizunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 30 na wanawake wakizunguka uwanja huo mara 25 na baada ya mashindano washindi kuanzia wa kwanza hadi wa 10 wamejinyakulia zawadi ya fedha taslimu na medali.
Mshindi wa Kwanza Mbio za Baiskeli za Kilomita 150 (Shinyanga- Isaka) alikuwa Gelard Nkonda kutoka Shinyanga aliyejinyakulia kitita cha shilingi milioni 1 na medali,mshindi wa pili Rashid Hamis kutoka Arusha aliyeondoka na kitita cha sh. 700,000/= na medali,mshindi wa tatu George Izengo kutoka Shinyanga aliyepata zawadi ya Shilingi 500,000/= na medali huku washindi kuanzia wan ne hadi 10 wakipata zawadi ya shilingi 200,000/- na medali kila mmoja.
Kwa upande wa mbio za kilomita 80 (Shinyanga – Kituli) mshindi wa kwanza ni Mwigulu Mdogo aliyepata zawadi ya shilingi 400,000/- na medali, wa pili Dotto Mahega (sh. 200,000/- na medali), mshindi wa tatu Mwendokasi Kalikali (Sh. 100,000/= na medali) na washindi wa nne hadi namba 10 wakiondoka na kifuta jasho cha shilingi 30,000/- na medali kila mmoja.
Aidha kwa upande wa mbio fupi za wanawake (kuzunguka uwanja wa Kambarage mara 25) mshindi wa kwanza alikuwa Futi mbili Richard aliyeondoka na kitita cha shilingi 200,000/= na medali,mshindi wa pili Modester Kashinje (sh. 100,000/- na medali, wa tatu Grace Nchambi (sh . 50,000/= na medali huku mbio za wazee wanaume (kuzunguka uwanja wa Kambarage mara 30) mshindi wa kwanza akiwa ni Sambo wa Sambo aliyepata zawadi ya sh. 200,000/= na medali,wa pili Kabaya Clement (sh. 100,000/- na medali, mshindi wa tatu Dotto Clement (sh. 50,000/- na medali).
Wakati mbio za baiskeli zikiendelea zoezi la uchangiaji wa damu salama lilikuwa linaendelea uwanjani huku mechi kali kati ya Timu ya mpira wa miguu ya Benki ya CRDB na Bwalo Gymnastic Centre ikichezwa uwanjani ambapo CRDB waliwababua Bwalo Gymnastic Centre bao 4-1 ambapo washindi na walioshindwa walipata zawadi ya mbuzi watatu ambao waliwachoma na kula nyama choma.
Katika maadhimisho hayo,pia Benki ya CRDB kwa kushirikiana na wadau wake wakiwemo Sanlam General Insurance, Kampuni ya Jambo Food Products, NIC wametoa msaada Viakisi Mwanga ‘Reflectors’ zenye thamani ya shilingi milioni 3.9 kwa ajili ya waendesha bodaboda mkoa wa Shinyanga waliopo kwenye vituo 35 vilivyosajiliwa kupitia ofisi ya Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza wakati wa Maadhimisho hayo, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ameipongeza Benki ya CRDB kwa ubunifu mkubwa katika shughuli mbalimbali lakini kwa ushirikiano inaotoa kwa serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo.
“Nawashukuru sana Benki ya CRDB kwa kuifanya siku ya leo kuwa ya Furaha badala ya majonzi tukimkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hatutakiwa kulia bali tunatakiwa kusherehekea mambo mazuri yaliyofanywa na baba wa Taifa ambaye nae pia alipenda kuendesha baiskeli”,alisema Telack.
“Wananchi wa Shinyanga mmewapa furaha wananchi,tangu asubuhi kila mahali walipopita waendesha baiskeli kuanzia hapa uwanja wa CCM Kambarage hadi Isaka,wananchi wamejitokeza kwa wingi kuangalia mbio za baiskeli. Hakika mbali na kuleta furaha pia mmewajenga vijana walioshiriki mbio za baiskeli kuwa na nguvu na wakakamavu. Hizi mbio za baiskeli siyo lelemama, Niwapongeze sana washiriki wote wa mbio za baiskeli”,aliongeza Telack.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa, aliwapongeza wananchi wote waliojitokeza kuchangia damu salama na kufanikisha kupatikana kwa uniti 140 za damu akibainisha kuwa wameokoa maisha ya wananchi wenye uhitaji wa damu na kuwaomba wananchi kuendelea kuchangia damu.
Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui alisema lengo la kuandaa mashindano hayo ya mbio za baiskeli na kuendesha zoezi la uchangiaji damu salama kuwa ni kuadhimisha Kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini pia kama sehemu ya mwendelezo wa kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Pamui aliwashukuru wadau walioungana na Benki ya CRDB katika maadhimisho hayo ambao ni Jambo Food Products CO.LTD,East African Spirit (T) Ltd, Fresho Investment Co. Ltd , Jielong Holdings Co. Ltd, Doctors With Africa,Tanzania Red Cross, Sanlam General Insurance, Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Kitengo Cha Damu Salama,Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga na Karena Hotels Ltd.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 21 tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere leo katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga maadhimisho ambayo yameenda sanjari Zoezi la Uchangiaji Damu na Mashindano ya Mbio za Baiskeli yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa wabunifu wa shughuli mbalimbali za maendeleo.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akielezea lengo la mashindano ya mbio za baiskeli na uchangiaji damu salama.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui (kulia), Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney (katikati) na Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana wakifurahia jambo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwashukuru Benki ya CRDB kwa kuandaa mashindano ya Baiskeli na kuwapongeza wananchi waliojitokeza kuchangia damu salama.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza
Meneji wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akiteta Jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko (kulia).
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui na Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana wakiwa wakijiandaa kuandesha baiskeli
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akizungumza na waendesha baiskeli kutoka Kahama maarufu Matambuu
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za baiskeli
Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru akifungua rasmi mashindano ya mbio za baiskeli
Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Africanus Sulle akiwaasa waendesha baiskeli kuwa makini barabarani/kuzingatia usalama barabarani wanapoendesha baiskeli
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akiendesha baiskeli wakati wa uzinduzi wa mbio za baiskeli
Waendesha baisekeli wakianza kutimua vumbi mjini Shinyanga kuelekea Isaka (KM 150)
Mshindi wa Kwanza Mbio za Baiskeli za Kilomita 150 (Shinyanga- Isaka) Gelard Nkonda akirejea Shinyanga Mjini kutoka Isaka
Washiriki mbio za baiskeli za km 150 (Shinyanga - Isaka) wakirejea Shinyanga Mjini
Washiriki wa mbio za Baiskeli wakirejea Shinyanga Mjini kutoka Isaka
Wananchi wakifuatilia mbio za baiskeli
Wananchi wakifuatilia mbio za baiskeli
Wadau wa mbio za baiskeli wakiwa eneo la tukio
Wapenzi wa mbio za baiskeli wakifuatilia mbio za baiskeli
Wadau wa mbio za baiskeli wakifuatilia mbio za baiskeli
Wadau wa mbio za baiskeli wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Washiriki wa mbio za baiskeli kilomita 80 (Kutosha Shinyanga kwenda Kituli na kurudi) wakijiandaa kuanza kutimua vumbi.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akiwapa neno washiriki wa mbio za baiskeli km 80
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Baiskeli mkoa wa Shinyanga, Kashi Salula akizungumza na waendesha baiskeli kabla mashindano hayajaanza rasmi
Mashindano ya mbio za baiskeli kutoka Shinyanga Mjini kuelekea Kituli (Km 80) yalivyoanza katika uwanja wa CCM Kambarage
Mashindano ya mbio za baiskeli kuelekea Kituli
Mashindano ya mbio za baiskeli kundi la wazee kuzunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 30 yakiendelea
Mshindi wa kwanza kundi la wazee akionesha mbwembwe wakati akihitimisha mbio za baiskeli
Mashindano mbio za baiskeli kundi la wanawake yakiendelea
Meza kuu wakifurahi burudani ya mbio za baiskeli kundi la wanawake
Meza kuu wakifuatilia mbio za baiskeli katika uwanja wa CCM Kambarage
Wananchi wakifuatilia mbio za baiskeli katika uwanja wa CCM Kambarage
Wananchi wakifuatilia mbio za baiskeli
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack kabla ya kuanza kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya mbio za baiskeli.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akijiandaa kumvalisha Medali na kumkabidhi kitita cha shilingi Milioni moja Mshindi wa Kwanza Mbio za Baiskeli za Kilomita 150 (Shinyanga- Isaka) Gelard Nkonda kutoka Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akimvalisha Medali na kumkabidhi shilingi laki 7 mshindi wa pili mbio za masafa marefu Rashid Hamis kutoka Arusha
Mshindi wa tatu George Izengo kutoka Shinyanga aliyepata zawadi ya Shilingi 500,000/= na medali akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akimkabidhi mshindi wa kwanza mbio fupi za wanawake (kuzunguka uwanja wa Kambarage mara 25) Futi mbili Richard kitita cha shilingi 200,000/= na medali.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akimkabidhi mshindi wa pili mbio fupi za wanawake (kuzunguka uwanja wa Kambarage mara 25)Modester Kashinje (sh. 100,000/- na medali.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akimkabidhi mshindi wa tatu mbio fupi za wanawake (kuzunguka uwanja wa Kambarage mara 25) Grace Nchambi (sh . 50,000/= na medali).
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akizungumza wakati akijiandaa kukabidhi medali kwa wadau mbalimbali walioshiriki/waliofanikisha maadhimisho ya Nyerere Day mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akimvalisha medali Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akishikana mkono na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akimvalisha medali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akimvalisha medali Mwakilishi wa Sanlam General Insurance, Tamari Mbise
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akishikana mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Baiskeli mkoa wa Shinyanga Kashi Salula baada ya kumvalisha medali
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akimvalisha medali Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Shinyanga & Simiyu, Dkt. Emmanuel Makala.
Wadau wakiwa jukwaa kuu
Askofu Makala akiwa na mke wake
Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akiangalia Medali kabla ya kuvalishwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui (kulia).
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Saidi Pamui akizungumza wakati wa zoezi la kugawa Viaksi Mwanga
Mwakilishi
wa Sanlam General Insurance , Tamari Mbise akizungumza wakati wa kukabidhi
Viaksi Mwanga kwa ajili ya waendesha bodaboda
Meneja
wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akikabidhi Viaksi Mwanga kwa
Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga Africanus Sulle kwa ajili ya waendesha bodaboda mkoa wa
Shinyanga
Mkuu
wa Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga Africanus Sulle akiwashukuru wadau kwa kutoa msaada wa
viaksi mwanga kwa waendesha bodaboda
Awali Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru akizungumza kabla ya mchezo wa mpira wa miguu kati ya Benki ya CRDB na Bwalo Gymnastic Centre
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru na viongozi wa Benki ya CRDB akipiga picha na kikosi cha timu ya Benki ya CRDB
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru na viongozi wa Benki ya CRDB akipiga picha na kikosi cha timu ya Bwalo Gymnastic Centre
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru na viongozi wa Benki ya CRDB akipiga picha na kikosi cha timu ya Benki ya CRDB na Bwalo Gymnastic Centre
Kikosi cha timu ya Benki ya CRDB na Bwalo Gymnastic Centre wakisimama kwa muda wa dakika 1 kumkumbuka Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kabla ya kuanza mechi
Mchezo kati ya Timu ya Benki ya CRDB na Bwalo Gymnastic Centre ukiendelea ambapo CRDB waliibuka washindi
Mchezo unaendelea
Sehemu ya wafanyakazi wa Tanzania Redcross wakiwa katika uwanja wa CCM Kambarage
Maafisa kutoka Kitengo cha Damu Salama hospitali ya Mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Dr. Joel ( wa pili kulia) wakijiandaa kuanza kuwahudumia wananchi waliojitolea kuchangia damua
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakichangia damu salama
Mmoja wa wananchi akiwa katika banda la Damu salama akijiandaa kuchangia damu
Zoezi la kuchangia damu salama likiendelea
Wananchi wakiendelea kuchangia damu salama
Sehemu ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye maadhimisho ya Nyerere Day
Askofu wa kanisa la KKKT, Dk. Emmanuel Makala akiwa na mke wake wakati wakichangia damu salama
Zoezi la kuchangia damu salama likiendelea
Zoezi la kuchukua taarifa za wachangiaji damu salama likiendelea kabla ya kuchangia damu salama
Dr. Joel akimpima wingi wa damu Meneja Biashara Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Idd wakati wa zoezi la uchangiaji damu.
Wafanyakazi wa Kampuni ya East Africa Spirit (T) LTD wakiwa katika banda lao
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa katika banda lao
Zoezi la uchangiaji damu salama likiendelea
Sehemu ya damu ilichangiwa na wananchi
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB akichangia damu salama
Wadau wa mbio za baiskeli wakiwa katika uwanja wa CCM Kambarage
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Halima Rashid akizungumza wakati wa maadhimisho ya Nyerere Day
Mwakilishi wa Kampuni ya East Africa Spirit (T) LTD, Erick akizungumza wakati wa maadhimisho ya Nyerere Day
Mwakilishi wa Doctors With Africa akizungumza
Mwakilishi wa Tanzania Redcross akizungumza
Mwakilishi wa Karena Hotels Ltd, bwana Juma akizungumza
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Baiskeli mkoa wa Shinyanga, Kashi Salula akizungumza
Mratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza mkoa wa Shinyanga, Dk. Gladness Mutayunwa akitoa taarifa ya kiwango cha damu iliyopatikana wakati wa uchangiaji damu maadhimisho ya Nyerere Day kuwa ni Uniti 140
Wadau wakiwa eneo la tukio
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiongozana na viongozi mbalimbali kwenda kutembelea mabanda ya wadau waliojitokeza na kushiriki katika maadhimisho ya Nyerere Day
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa katika banda la Kampuni ya Jambo Food Products Ltd.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa katika banda la Kampuni ya East Africa Spirit (T) LTD
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa katika banda la Kampuni ya East Africa Spirit (T) LTD akiangalia kinywaji cha Diamond Rock
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa katika banda la TANESCO
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa katika banda la Benki ya CRDB
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa katika banda la Benki ya CRDB
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa katika banda la Benki ya CRDB
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa katika banda la Kitengo cha Damu Salama kutoka Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa katika banda la Kitengo cha Damu Salama
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa katika banda la Redcross
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa katika banda la Doctors with Africa
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa katika banda la Doctors with Africa.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog