Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dkt. Severine Lalika, akizungumza kwenye Semina ya wastaafu iliyoandaliwa na benki ya CRDB mkoani Mwanza katika ukumbi wa hoteli ya Gold Crest.
Benki ya CRDB imeendesha semina ya siku moja kwa wastaafu mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango maalum wa uwezeshaji kwa wastaafu ambao ulizinduliwa na benki hiyo mwishoni mwa mwezi Septemba. Akizungumza katika semina hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dkt. Severine Lalika aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuwawezesha wazee huku akielezea azma ya serikali ni kuhakikisha inatengeneza maisha bora kwa wastaafu wote nchini kwa kuwajengea mazingira endelevu ya kujiingizia kipato
''Naipongoeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa wabunifu kwa kuja na wazo hili la kuwakutanisha wastaafu ili kujadili kwa pamoja fursa zinazopatikana katika benki hii ukizingatia kundi hili la wateja limekuwa likisahaulika''amesema Dkt. Lakila.
Aidha amesema kuwa CRDB imefanya jambo kubwa kwa kufanya semina kwa wastaafu maana ni kitu kigeni kwa benki ya mikopo kuwakutanisha wastaafu kwa kujadili pamoja na kuwapa mbinu na ujuzi kwa kunijiendeleza kimaendeleo kwa kuongeza kipato.
Dkt. Lakila amewapongeza wastaafu wote walioitikia wito kwa kuja kujifunza mafunzo masula ya kibenki zitolewazo na Benki ya CRDB imani yangu baada ya kongamano hili kutakuwa na mabadiliko makubwa katika utunzaji na uwekaji wa fedha pamoja na masuala ya mikopo.
''Leo ni siku muhimu kwa Benki ya CRDB kwa kutukusanya hapa hivyo naamini baada ya mafunzo hayo tutapata elimu jinsi ya kuwekeza na kutunza masuala ya mikopo katika kuboresha maisha yetu''amesema Dkt. Lakila.
Dkt. Lakila ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuanzisha na kutekeleza mpango huu wa uwezeshaji kwa wastaafu wenye lengo la kuleta faraja na kuwasaidia wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbalimbali ya kimaisha zote tumekuwa tukiona changamoto hivyo mpango huu utaleta tumaini jipya.
Meneja wa Uwezeshaji kwa Wateja Benki ya CRDB, Crispin Sichwale akizungumza juu ya fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa wastaafu katika semina iliyoandaliwa na benki hiyo mkoani Mwanza.
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya CRDB Uwezeshaji kwa Wateja, Chrispin Sichwale alisema mpango huo wa uwezeshaji kwa wastaafu anajumuisha fursa za kujiwekea akiba, uwekezaji, pamoja na uwezeshaji wa kifedha kwa wastaafu. Sichwale alisema hivi karibuni Benki hiyo imezindua huduma za akaunti maalum ya wastaafu “Pension Account” na huduma ya uwezeshaji wa kifedha kwa wastaafu kidijitali “Pension Advance” kupitia huduma ya SimBanking App, ambapo wastaafu hupata mkopo bure.
“Ninajivunia kuwajulisha kuwa hadi leo hii tukiwa tunazindua mpango huu wa uwezeshaji wastafu, tayari wastaafu zaidi ya 19,000 wameshafungua akaunti hii na wanafurahia huduma zetu,” alisema Sichwale huku akibainisha kuwa kupitia akaunti hiyo wastaafu wanapewa TemboCard inayowawezesha kupata huduma kwa CRDB Wakala na ATM zote nchi nzima.
Sichwale alisema kupitia mpango huo wa uwezeshaji kwa wastaafu benki hiyo pia imejipanga kuendelea kutoa mikopo kwa wastaafu ili kuwawezesha kuendeleza biashara na miradi yao ya maendeleo na hivyo kupunguza ukali wa maisha ya kila siku. Kupitia mkopo huo Wastaafu wanaweza kukopa kuanzia shilingi milioni 1 hadi shilingi milioni 100 kwa kipindi cha mwaka 1 hadi 7.
Social Plugin