Elisha Elia enzi za uhai wake.
Mtangazaji wa TBC, Elisha Elia amefariki Dunia leo Jumamosi Oktoba 24,2020 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.
Hii ni sehemu ya Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba:
"Mkurugenzi Mkuu wa TBC,Dkt. Ayub Rioba anasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzetu, Mwandishi wa Habari Elisha Elia, kilichotokea tarehe 24/10/2020 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Taarifa zaidi zitatolewa".
R.I.P Elisha Elia.
Social Plugin