Angalia Picha : KATAMBI AFANYA MKUTANO MKUBWA WA KAMPENI KAMBARAGE...ANKO MWENDA ATAKA 'TATU BILA' OKTOBA 28

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kambarage wakati akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa mbunge.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi ameendelea na kampeni zake za kunadi sera za CCM na kuomba wananchi wamchague kuwa mbunge ambapo leo Jioni alikuwa katika kata ya Kambarage.

Akuzungumza leo Jumatano Oktoba 21,2020 katika mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanachama wa CCM katika kata ya Kambarage, Katambi amewaomba wananchi wamchague kuwa mbunge kwani anayo dhamira ya kweli kuwaletea maendeleo.

“CCM ndiyo Kambi ya Maendeleo. Mchagueni Katambi. Mimi siyo Boya, nipeni kura ili niwaletee maendeleo”,amesema Katambi.

Amesema miongoni mwa vipaumbele vyake ni pamoja na kujenga barabara,mitaro na makalavati,ujenzi wa soko la Kisasa, Stendi ya mabasi ya kisasa na ujenzi wa maegesho ya magari ‘Lori Park’,kuboresha sekta ya afya,elimu,kilimo na ufugaji na maji.

“Ndugu zangu chagueni mbunge anayejitambua,achaneni na hao wanaotuchelewesha. Atayeikomboa Shinyanga ni Mimi Katambi nisiye na Kitambi”,ameongeza Katambi.

Katika hatua nyingine mbali na kuomba kura pia amewaomba wananchi kumchagua Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,madiwani wa CCM akiwemo  Hassani Mwendapole katika kata ya Kambarage.

Kwa upande wao, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Gulam na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Dotto Joshua wamewaomba wananchi kuendelea kuiamini CCM hivyo wawachague wagombea wa CCM ili kuwaletea maendeleo.

Naye Mgombea Udiwani kata ya Kambarage, Hassan Mwendapole maarufu Anko Mwenda  amewaomba wananchi wamchague tena kuwa diwani ili kukamilisha mambo mbalimbali aliyokuwa hayajamilisha kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

“Oktoba 28 naomba tupige Tatu Bila…tatu bila maana yake ni kuchagua wagombea wote wa CCM. Nichagueni kuwa diwani, mchagueni Katambi kuwa mbunge na Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Rais”,amesema Mwendapole.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kambarage wakati akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa mbunge. Picha zote na Kadama Malunde 1 blog
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga ,Patrobas Katambi akiomba kura kwa wananchi
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kambarage wakati akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa mbunge.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kambarage wakati akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa mbunge.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kambarage wakati akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa mbunge.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kambarage wakati akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa mbunge.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akimuombea kura mgombea Udiwani kata ya Kambarage, Hassan Mwendapole (kushoto)
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akielekeza wananchi namna ya kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28,2020.

Wanachama wa CCM na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi wakishangilia
Wananchi wakishangilia
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Gulam akiwaombea kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi akiwemo Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mgombea Udiwani kata ya Kambarage, Hassan Mwendapole maarufu Anko Mwenda  akiwaomba wananchi wamchague tena kuwa diwani ili kukamilisha mambo mbalimbali aliyokuwa hayajamilisha kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Kada wa CCM Kashi Salula ambaye alikuwa miongoni wa watia nia kugombea ubunge Jimbo  la Shinyanga Mjini akiwaombea kura wagombea wa CCM.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Dotto Joshua akiwaombea kura wagombea wa CCM.
Wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni

Wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post