Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kambarage wakati akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa mbunge. Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi ameendelea na kampeni zake za kunadi sera za
CCM na kuomba wananchi wamchague kuwa mbunge ambapo leo Jioni alikuwa katika
kata ya Kambarage.
Akuzungumza leo Jumatano Oktoba 21,2020 katika mkutano wa
kampeni uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanachama wa CCM katika kata ya
Kambarage, Katambi amewaomba wananchi wamchague kuwa mbunge kwani anayo dhamira
ya kweli kuwaletea maendeleo.
“CCM ndiyo Kambi ya Maendeleo. Mchagueni Katambi. Mimi siyo
Boya, nipeni kura ili niwaletee maendeleo”,amesema Katambi.
Amesema miongoni mwa vipaumbele vyake ni pamoja na kujenga
barabara,mitaro na makalavati,ujenzi wa soko la Kisasa, Stendi ya mabasi ya
kisasa na ujenzi wa maegesho ya magari ‘Lori Park’,kuboresha sekta ya afya,elimu,kilimo
na ufugaji na maji.
“Ndugu zangu chagueni mbunge anayejitambua,achaneni na hao
wanaotuchelewesha. Atayeikomboa Shinyanga ni Mimi Katambi nisiye na Kitambi”,ameongeza
Katambi.
Katika hatua nyingine mbali na kuomba kura pia amewaomba
wananchi kumchagua Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,madiwani wa CCM akiwemo Hassani
Mwendapole katika kata ya Kambarage.
Kwa upande wao, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,
Abubakari Gulam na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Dotto Joshua
wamewaomba wananchi kuendelea kuiamini CCM hivyo wawachague wagombea wa CCM ili
kuwaletea maendeleo.
Naye Mgombea Udiwani kata ya Kambarage, Hassan Mwendapole
maarufu Anko Mwenda amewaomba wananchi
wamchague tena kuwa diwani ili kukamilisha mambo mbalimbali aliyokuwa
hayajamilisha kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.
“Oktoba 28 naomba tupige Tatu Bila…tatu bila maana yake ni
kuchagua wagombea wote wa CCM. Nichagueni kuwa diwani, mchagueni Katambi kuwa mbunge na
Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Rais”,amesema Mwendapole.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kambarage wakati akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa mbunge. Picha zote na Kadama Malunde 1 blog
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga ,Patrobas Katambi akiomba kura kwa wananchi
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kambarage wakati akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa mbunge.

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akimuombea kura mgombea Udiwani kata ya Kambarage, Hassan Mwendapole (kushoto)
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi akielekeza wananchi namna ya kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28,2020.

Wanachama wa CCM na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi wakishangilia
Wananchi wakishangilia
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Gulam akiwaombea kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi akiwemo Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mgombea Udiwani kata ya Kambarage, Hassan Mwendapole maarufu Anko Mwenda akiwaomba wananchi wamchague tena kuwa diwani ili kukamilisha mambo mbalimbali aliyokuwa hayajamilisha kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Kada wa CCM Kashi Salula ambaye alikuwa miongoni wa watia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini akiwaombea kura wagombea wa CCM.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Dotto Joshua akiwaombea kura wagombea wa CCM. Wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni
Social Plugin