Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza Dkt.John Pombe Magufuli kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mshindi wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 12,516,252, akifuatiwa na Tundu Lisu wa CHADEMA mwenye kura 1,933,271 huku Bernard Membe kutoka ACT-Wazalendo akiwa amepata kura 81,129.
Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema kuwa jumla ya waliojiandikisha ni 29,754,669, na kura halali zilizopigwa ni 14,830,195 huku kura 261,755 zikikataliwa.
”Tume inamtangaza Dkt. Magufuli kuwa Rais wa Tanzania amepata kura nyingi halali kuliko wagombea wengine wote na tunamtangaza Mama Samia Hassan Suluhu kuwa Makamu wa Rais wa Tanzana”,amesema Jaji Mstaafu Kaijage
Jaji Mstaafu Kaijage amesema kuwa Rais Mteule pamoja na makamu wake watakabidhiwa cheti cha ushindi siku ya Jumapili.
Wapiga kura waliojitokeza Kura - 15,910,950
Idadi ya kura halali 14,830,195
Idadi ya Kura zilizokataliwa 261,755
Kura Walizopata Wagombea
Dkt John Pombe Magufuli CCM
Kura - 12,516,252
Leopard Lucas Mahona NRA
Kura -8787
John Paul Shibuda ADA- TADEA
Kura - 33,086
Muttamwega Mgaywa SAU
Kura - 14,922
Cecilia Augustino Mmanga (Demokrasia Makini)
Kura - 14,556
Maganja Yeremia Kurwa (NCCR)
Kura - 19,969
Lipumba Ibrahim Haruna (CUF)
Kura - 72,885
Philipo John Fumbo (DP)
Kura - 8,283
Membe Benard Kamillius(ACT)
Kura - 81,129
Queen Curthibert Sendiga (ADC)
Kura - 7627
Twalib Ibrahim Kadege (UPDP)
kura - 6194
Rungwe Hashim Spunda (CHAUMMA)
Kura - 32,878
Mazrui Alfan Mohamed (UMD)
Kura - 3721
Seif Maalim Seif (AAFP)
Kura - 4,635
Lissu Tundu Antiphas Mughwai (CHADEMA)
Kura - 1,933,271