Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MHASIBU MKUU WIZARA YA MAJI AKAGUA MIRADI YA MAJI KAHAMA..ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI



Mhasibu Mkuu kutoka Wizara ya Maji Ahadi Msangi, akizungumza na wananchi wa Isaka, kwenye kituo cha kuchotea maji safi na salama kutoka mradi wa maji wa Ziwa Victoria.

Na Marco Maduhu - Kahama.
Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Maji ikiongozwa na Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ahadi Msangi, wamefanya ya ukaguzi ya Miradi ya Maji Mkoani Shinyanga ambapo wamekagua utekelezaji wa miradi ya maji wilaya ya Kahama.

Baada ya kutembelea miradi hiyo ya Maji leo Msangi ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wake, huku akitoa wito kwa wananchi wajiunge na mtandao wa maji, ili wapate huduma ya maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria.

Watalaamu hao wamekagua Utekelezaji wa mradi wa maji, Isaka- Kagongwa, ambao tayari umeshaanza kutoa huduma ya maji lakini wamekagua mradi wa Ngogwa –Kitwana na Mbulu- Mwamva, ambayo ipo kwenye hatua ya ukamilishaji.

Amesema amefurahishwa na utekelezaji wa miradi hiyo ya maji, ambayo itaondoa changamoto ya wananchi kutumia maji ambayo siyo salama kwa afya zao, kwa kupata huduma ya maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria, na kuwataka wajiunge na mtandao wa maji ili wapate huduma hiyo.

“Lengo la ziara yetu ni kukagua miradi ya maji ambayo inatekelezwa chini ya Wizara ya Maji, na nimeridhishwa na utekelezaji wake, ila kuna changamoto ya idadi ndogo ya wananchi wa Kagongwa na Isaka kujiunga na mtandao wa maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria, naomba wajiunge ili wafurahie huduma hii ya maji,” amesema Msangi.

Naye Mhandisi Sayi Kapela kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama na Shinyanga (KASHWASA), amesema wakazi wa Isaka wapo 16,000, lakini waliojiunga na mtandao wa maji ni 446, ambapo Kagongwa ina wakazi 35,000, lakini waliojiunga ni 371, idadi ambayo ni ndogo huku mradi huo ukigharimu Shilingi Bilioni 24.7.

Kwa upande wake, Meneja ufundi kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA), Luchanganya Paulo, amesema tatizo walilobaini wananchi kutojiunga kwa wingi na mtandao wa Maji Ziwa Victoria, ni kuendelea kutumia maji ya visima vyao, ambavyo walikuwa wamevichimba hapo awali.

Nao baadhi ya wananchi ambao wamejiunga na mtandao wa maji akiwemo Catherine Silvester, wameishukuru Serikali kwa kuwatekelezea mradi huo, ambao umewasaidia kuondokana na magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji machafu, pamoja na kupoteza muda wa kufanya shughuli za kimaendeleo kwa kutafuta maji safi na salama umbari mrefu.



TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mhasibu Mkuu Wizara ya Maji Ahadi Msangi, akizungumzia ziara yake na kufurahishwa na utekelezaji wa miradi ya maji Kahama leo Jumanne Oktoba 6,2020. Picha na Marco Maduhu


Meneja Makala wa Maji vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga Juliety Payovela, akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji.
Mhandisi Sayi Kapela kutoka (KASHWASA) akielezea namna mradi wa maji ulivyotekelezwa wa Isaka na Kagongwa.
Meneja ufundi kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA), Luchanganya Paulo, akielezea namna wanavyotekeleza miradi ya maji kwa kushirikiana na mamlaka zingine za maji ikiwamo SHUWASA.
Mwananchi Catherine Silvester, akielezea namna wanavyonufaika na mradi wa maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria.

Mhasibu Mkuu Wizara ya Maji Ahadi Msangi, akizungumza na wananchi wa Isaka, kwenye kituo cha kuchotea maji safi na salama kutoka mradi wa maji wa Ziwa Victoria.

Wananchi wa Isaka wakichota maji safi na salama kutoka mradi wa maji ya Ziwa Victoria.

Muonekano wa Tenki la kuhifadhia maji kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Kitwana ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.

Ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maji ukiendelea.

Ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maji ukiendelea.
Mabomba ya kusambaza maji.

Muonekano wa Matenki ya kuhifadhia maji na kuyasambaza Isaka na Kagongwa.


Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Maji Ahadi Msangi, katikati, akipiga picha ya pamoja na watumishi wa mamlaka za maji KUWASA, SHUWASA, pamoja na Meneja Wakala wa Maji vijijini Mkoa wa Shinyanga RUWASA, Juliety Payovela.

Na Marco Maduhu- Kahama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com