Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : SALOME MAKAMBA ATIKISA MJI WA SHINYANGA AKIOMBA KURA ...MAELFU WAFURIKA SOKO KUU

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba 'Ng'wana O Shimba'  ameendelea na kampeni za kuomba wananchi wamchague kuwa mbunge katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28,2020 ambapo jioni hii alikuwa katika Soko Kuu la Mjini Shinyanga lililopo katika kata ya Mjini.

Mkutano huo wa Salome Makamba ni wa 42 tangu aanze kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Shinyanga Mjini umehudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanachama wa CHADEMA ambapo Makamba amewaomba wananchi wamchague kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ili kuwaletea maendeleo wananchi akibainisha kuwa CHADEMA inazingatia haki,uhuru na maendeleo ya watu.

Salome Makamba amewaomba wananchi kumchagua Tundu Lissu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wagombea wa Ubunge na Udiwani kupitia CHADEMA katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba akizungumza katika mkutano wa kampeni ulifanyika katika eneo la Soko Kuu la Mjini Shinyanga akiomba wananchi wamchague kuwa mbunge,Tundu Lissu kuwa Rais na madiwani wa CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba akinadi sera za CHADEMA
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika eneo la Soko Kuu la Mjini Shinyanga 

Wananchi wakimsikiliza Salome Makamba
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika eneo la Soko Kuu la Mjini Shinyanga 
Wanachama wa CHADEMA wakifuatilia mkutano wa kampeni
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika eneo la Soko Kuu la Mjini Shinyanga 
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba akiomba wananchi wamchague kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba akiomba kura kwa wananchi
Wananchi wakifuatilia mkutano

Mwenyekiti wa  CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi ambaye pia ni Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo akimuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba na Mgombea Udiwani kata ya Mjini, Nicholaus Luhende.
Mwenyekiti wa  CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi ambaye pia ni Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo akizungumza wakati akimuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba (kushoto) na Mgombea Udiwani kata ya Mjini, Nicholaus Luhende (katikati).
Mgombea Udiwani kata ya Mjini, Nicholaus Luhende akisalimiana na wananchi
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA, Salome Makamba akifurahia zawadi ya Viatu alivyopewa na mmoja wa wauza viatu aliyehudhuria mkutano huo wa kampeni za Salome Makamba
Wananchi na wanachama wa CHADEMA wakimsindikiza Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba kutoka eneo la Soko Kuu Mjini Shinyanga kuelekea katika ofisi za CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini baada ya mkutano wa kampeni kumalizika
Wananchi na wanachama wa CHADEMA wakimsindikiza Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba kutoka eneo la Soko Kuu Mjini Shinyanga kuelekea katika ofisi za CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini baada ya mkutano wa kampeni kufungwa.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com