Mgombea urais kupitia CUF Profesa Ibrahim Lipumba.
**
Pia mgombea urais huyo amewaahidi wakulima wa matunda mkoani Tanga kuwa atahakikisha kuwa anawajengea viwanda vya kutengeneza juisi kupitia matunda wanayozalisha ili waweze kupata masoko nje ya nchi na hatimaye waweze kukuza uchumi wao.
Akizungumza na wananchi wa Mombo na Bungu wilayani Korogwe, Profesa Lipumba amesema hivi sasa hakuna utaratibu mzuri wa kuweza kuimarisha masoko ya wakulima wa mbogamboga wakapata masoko ya kuuzia mazao yao.
Profesa Lipumba amesema kuwa mbogaboga ni moja kati ya mazao yanayohitajika katika nchi za Ulaya wakati wa majira ya baridi, ambayo yanaendelea hivi sasa kutokana na nchi hizo kutokubali kilimo cha mbogamboga wakati wa baridi na kulazimika kuagiza nchini Tanzania.
Aidha Prof. Lipumba ameongeza kuwa kipaumbele kingine kwenye serikali yake endapo wananchi watampa dhamani ni pamoja kuboresha mitaala ya elimu ikiwemo kuajiri walimu wengi zaidi kwa sababu hakuna maendeleo bila maendeleo.
Kwa upande wake mgombea mwenza kwa tiketi ya chama hicho Hamida Abdallah Huweish, akazungumzia lengo la chama hicho kutaka kushika dola ni kuwakomboa Watanzania.
Chama cha CUF kinaendelea kufanya mikutano mbalimbali ya kuomba kura za urais, wabunge na madiwani katika mikoa mbalimbali katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba 28 mwaka huu.
CHANZO - EATV