Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge akimnadi Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo Victor Mkwizu (kulia)
Na Suzy Luhende - Shinyanga
Mgombea udiwani kata ya Ngokolo Victor Mkwizu amewaomba wananchi wa kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga wamchague ili aweze kuondoa kero zilizopo ikiwa ni pamoja na barabara ya kutoka Mshikamano kuelekea makaburini katika mtaa wa Mageuzi.
Hayo ameyasema leo wakati akinadi sera zake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa wa Mageuzi kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ambapo alisema kero ya barabara inawatesa sana wananchi wa kata ya Ngokolo hivyo aliomba wamchague ili aweze kuiondoa kero hiyo.
Mkwizu amesema barabara hiyo ya kuelekea makaburi ya Mageuzi imekuwa ni tatizo kubwa kwani ikinyesha mvua baiskeli, pikipiki na Magari hayapiti yanakwama njiani wakati mwingine hata magari liyobeba maiti yanashindwa kufika Malaloni hivyo ataliweka kipaumbele kuliondoa tatizo hilo.
Pia amesema atakapochaguliwa atasikiliza mahitaji mbalimbali ya wananchi katika mataa yote na kuhakikisha anayapeleka sehemu husika ili yaweze kufanyiwa kazi na kutatuliwa.
Social Plugin